Pages

March 29, 2016

WAFANYABIASHARA WA MAFUTA WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZA UWEKEZAJI WA BOMBA LA MAFUTA LINALOGHRAIMU DOLA BILIONI NNE.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Justin Ntalikwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam l kuhusiana na Bomba la Gesi litakalokuwa likisafirisha kutoka Tanga kwenda uganda. 
Mwenyekit wa Chama cha wafanyabiashara wa mafuta nchini(NICOL), Gidion Kaunda akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya Katibu mkuu kuzungumzia bomba la mafuta la Tanga kwenda Uganda.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Justin Ntalikwa(aliye mbele) jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii. 
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa amesema kuwa wafanyabiahara wa mafuta wanafursa mbalimbali katika ujengaji wa bomba la mafuta kutoka Tanga hadi Uganda.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Profesa Ntalikwa amesema kuwa bomba la mafuta likianza mchakato wafanyabiashara wanaweza kuomba zabuni mbalimbali zitakazojitokeza.
Mradi wa ujenzi wa bomba hilo unagharimu dola za Kimarekani Bilioni Nne ambapo utaongeza ajira nyingi pamoja na kodi.
Amesema kuwa bomba hilo litajengwa nchini kwa asilimia 90 kutokana na amani iliyopo ukilinganisha na nyingine zilizo katika mradi huo.

Profesa Ntalikwa amesema kuwa kigezo cha kwanza cha kujenga bomba nchini ni kutokana na Bandari ya Tanga kuwa na kina kirefu cha kufanya kila meli kuweza kuingia hapo na tofauti bandari ya Mombasa nchini Kenya.
Amesema kutokana na vigezo vinaashiria kujengwa nchini licha ya kuwepo kwa majadiliano yanayoendelea juu ya bomba hilo litajengwa wapi.
Amesema kuwa nchi ya Kenya ndio inayofanya kuwa katika mchakato wa mwisho hivyo wenyewe ni watu wa kuangalia tu jinsi ya mradi utapofanyika.

Aidha Profesa Ntalikwa amesema kuwashirikisha wafanyabiashara wa mafuta ni kutaka kukujua fursa zilizo katika ujenzi wa bomba la mafuta wa kuweza kuomba zabuni.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...