Pages

March 30, 2016

MICHEZOTanzania shughuli tunayo June 4 na September 3


Siku zinazidi kusogea na matumaini ya Tanzania yanazidi kupungua kuhusu safari yaGabon mwaka 2017 katika michuano ya mataifa ya Afrika. Baada ya timu ya taifa yaChad kujiondoa katika michuano ya Mataifa ya Afrika na kuacha mtihani Kundi G lenye timu za TanzaniaMisri na Nigeria.
March 29 timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles iliondolewa na Misri katika mbio za kuwania kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2017 itakayofanyika Gabon,Nigeria ilitolewa baada ya kufungwa goli 1-0 katika mchezo wa marudiano.
_88991537_egyptnigeria
Jitihada za Ramadan Sobhy kuifungia Misri goli dakika ya 66 ndio zilizoiondoa Nigeriakwani hawakufanikiwa kusawazisha,  Nigeria inaaga mashindano hayo na nafasi pekee inabakia kwa Tanzania na Misri, kwani Nigeria imebakiza mchezo mmoja dhidi yaTanzania na hata ikishinda haitaweza kusonga mbele.
raaaaaa
Msimamo wa Kundi G ulivyo kwa sasa
Kazi imebakia kwa Tanzania kushinda mechi zake mbili dhidi ya Misri June 4 uwanja wa Taifa na Nigeria September 3 utachezwa Nigeria, kama Tanzania itashinda mechi zote mbili kwa idadi kubwa ya magoli, itakuwa imeizidi Misri kwa tofauti ya magoli. Nigeriaikiifunga Tanzania itakuwa inatimiza point 5 pekee.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...