KAMATI
ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu, imefanya ziara ya
kutembelea mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (Terminal Three- TBIII), jijini Dar es Salaam, Machi 29, 2016
ambapo awali wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Profesa Norman
Adamson Sigalla King, walipatiwa maelezo ya kina ya maendeleo ya mradi
huo unaohusisha jengo la kisasa la abiria na sehemu ya kuegesha ndege
kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria na sehemu ya maegesho ya magari.
Baada ya maelezo hayo ya kina yaliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, (TAA), Mhandisi George Sambali
akisaidiana na baadhi ya wakurugenzi wengine wa Mamlaka hiyo, wajumbe
hao walitembelea mradi huo na kujionea hatua mbalimbali za ujenzi ambapo
kwa sasa ujenzi umefikia karibu asilimia 60. Pichani, Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa TAA, Mhandisi George Sambali, (kushoto), akitoa maelezo kwa
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Norman Adamson Sigalla King,
(kulia), na baadhi ya wajumbe na maafisa wa TAA.
Mwenyekiti wa Kamati, akizungumza
Kaimu
Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha,
akizungumza na wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge kabla ya kutembelea mradi
Baadhi
ya wajumbe wa Kamati hiyo na maafisa wa TAA, wakisikiliza maelezo
yaliyokuwa yakitolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi George
Sambali (hayupo pichani)
Mkurugenzi
wa Mradi huo wa TBIII, Mhandisi Mohammed Millanga, (kulia), akitoa
maelezo ya maeneleo ya mradi huo. (kushoto) ni Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali Watu wa TAA, Laurent Mwigune
Mjumbe wa Kamati, Anna Richard Lupembe, akizungumza
Mjumbe
wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu, na Mbunge wa Fuoni,
Zanzibar, Abbas Ali Hassan Mwinyi, (kulia), akisalimiana na Mkurugenzi
wa Sheria na Mahusiano wa TAA, Ramadhan Maleta, na Mkurugenzi wa Utawala
na Rasilimali Watu, Laurent Mwigune (kushoto)
Mkurugenzi
wa Mradi huo wa TBIII, Mhandisi Mohammed Millanga(kushoto), akimueleza
Mwenyekiti wa Kamati, Profesa Sigalla, sehemu ya maegesho ya ndege
Mkurugenzi
wa Mradi huo wa TBIII, Mhandisi Mohammed
Millanga(kushoto), akimueleza Mwenyekiti wa Kamati, Profesa Sigalla,
(kulia kwake) na baadhi ya wajumbe na maafisa wa TAA, wakiongozwa na
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mhandisi Sambali, (wakwanza kulia), sehemu ya
maegesho ya ndege
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania, ATCL, Johnson Mfinanga akizungumzia hali ya shirika hilo
Afisa Mkuu wa Masoko wa TAA, Scholastica Mukanjanga, akizungumza
Mjumbe wa Kamati akizungumza
Mjumbe wa Kamati akizungumza
Mjumbe wa Kamati, Abass Ali Hassan Mwinyi, (katikati), akizungumza
Sehemu ya jengo la uwanja huo
No comments:
Post a Comment