Pages

March 22, 2016

Hizi hapa sentensi za Zitto baada ya kumwandikia Spika barua ya kujiuzulu

Gazeti la Mtanzania leo March 22 limeripoti kuhusu kamati za Bunge kutarajiwa kufanyiwa mabadiliko makubwa baada ya ripoti ya uchunguzi wa mwenendo wa wabunge kuwatuhumu baadhi yao kujihusisha na vitendo vya rushwa kutua mezani kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ameandika kupitia mtandao wa kijamii wa facebook kuwa….
>>>’Kuna tuhuma za rushwa dhidi ya Kamati mbalimbali za Bunge ikiwemo kamati ninayohudumu. Nimemwandikia Spika Kuomba Uchunguzi juu Ya tuhuma hizo na kwamba achukue hatua kali dhidi ya yeyote atakayekutwa kuhusika na vitendo vya rushwa. Nimejiuzulu Ujumbe wa Kamati ili Kutoa Nafasi Ya Uchunguzi Husika
zitto

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...