Pages

February 8, 2016

ZAIDI YA KAYA 60 KIWALALA NA MJIMWEMA ZIMEATHIRIKA NA MAFURIKO

Mafuriko Wilaya ya Lindi
Zaidi ya Kaya 60 za Vitongoji vya Kiwalawala na Mjimwema Kata ya Kitomanga Wilayani Lindi Zimeathiriwa na Mvua Zilizoambatana na Mafuriko Huku watu 94 wakifanikiwa Kuokolewa Kufuatia Jitihada za Halmashauri ya wilaya Ya Lindi kupeleka Boti kusaidia zoezi la Uokoaji.

Mvua hizo zilizonyesha Mwanzoni mwa wiki hii Tayari Maeneo mbalimbali ya wilaya Hiyo pamoja na Wilaya ya Kilwa kukosa sehemu za Kuishi huku jitihada za Kuokoa waliozungukwa na Maji zikiendelea.

Mafuriko Wilaya ya Lindi
Lindiyetu.com ilifika katika Maeneo Jirani na kijiji Cha Mjimwema jirani na Kitongoji wanachoishi wafugaji na Kushuhudia zoezi la Uokoaji Likiendelea na Ilifanikiwa Kuongea na Baadhi ya waliookolewa ambapo walieleza Jinsi walivyokutwa na Maafa hayo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Lindi Bi Oliva Vavunge akiongea na Lindiyetu.com wakati zoezi la Uokoaji likiendelea amewataka wananchi wote wanaoishi sehemu za mabondeni kuhama maramoja kwani Mvua hizo bado zinaendelea kunyesha kama ilivyotangazwa na mamlaka ya hali ya hewa nchini.
Mafuriko Wilaya ya Lindi
Diwani wa kata Ya Kitoanga alitoa ombi kwa Kitengo cha Maafa kutoa msaada wa haraka kwa wahanga hao.
Mafuriko Wilaya ya Lindi
Sambamba na Tukio Hilo Mkurugenzi Mtendaji pia amewataka wakazi wanaoishi katika Bonde la Mto Lukuledi Kuanza Kuondoka katika Bonde Hilo Ili kunusuru Maisha yao pamoja na Mali zao.
http://kickzacelebrity.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...