Pages

February 27, 2016

YANGA SC YAIFUNGASHA VIRAGO CERCLE DE JOACHIM LIGI YA MABINGWA AFRIKA KWA BAO 3-0 JIJINI DAR ES SALAAM

KLABU ya Yanga SC imesonga mbele kwa kuiondosha klabu ya Cercle de Joachim katika mashindano ya kombe la mabingwa wa afrika kwa jumla ya bao 3-0.


Cercle de Joachim ilikubali kipigo cha bao 1-0 katika uwanja wake wa nyumbani katika mchezo wa awali kabla ya kukubali tena kipigo cha bao bao 2-0 katika mchezo wa marudio uliochezwa leo uwanja wa taifa jijini Dar Es Salaam

Mshambuliaji Amis Tambwe alipachika bao dakika ya tatu kipindi cha kwanza kabla ya Thaban Scara Kamusoko aliyefunga bao la pili dakika ya 55 katika kipindi cha pili.

Katika mchezo wa awali Yanga SC ikiwa ugenini iliibuka na ushindi wa bao 1-0 bao lililopachikwa wavuni na Donald Ngoma na kufanya Yanga isonge mbele kwa jumla ya bao 3-0.

Kutokana na matokeo hayo Young Africans wanasubiri kucheza na mshindi kati ya klabu ya APR FC ya Rwanda ama Mbabane Swallows ya Swaziland ambapo katika mchezo wa awali APR walifungwa bao 1-0.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...