Watu
saba wameuwawa kwa kupigwa risasi akiwemo mtoto wa miaka nane huku
wengine kadhaa wakijeruhiwa katika tukio la mauaji lililotokea huko
Kalamazoo, Michigan nchini Marekani jana usiku.
Polisi
wamesema mtuhumiwa huyo amekamatwa kwenye gari linaloshabihiana na
lililotumiwa mshambuliaji, ambapo pia bunduki ilipatikana kwenye gari
hilo.
Mtuhumiwa huyo mzungu mwanaume mwenye umri wa miaka 45, ni mkazi wa kaunti ya Kalamazoo, imeelezwa alijisalimisha bila ya purukushani
No comments:
Post a Comment