Kiongozi Mkuu wa mfuko wa PPF (Director General) William Erio (kushoto) akipokea michoro ya jengo jipya la PPF Jijini Arusha kutoka kwa Mbunifu na Msimamizi Mkuu wa mradi wa ujenzi wa jengo hilo, Arch. Dudley Mawalla (kulia) kutoka kampuni ya MD Consultancy Ltd ya Dar es Salaam, katika hafla fupi ya makabidhiano rasmi ya jengo kutoka kwa mkadarasi wa kichina CREJ (EA) Ltd. Anayeshuhudia Katikati ni Injinia wa Miradi ya PPF, Injinia Marko Kapinga.
DG William Erio (pichani juu) ameisifu timu yote iliyoshiriki kufanikisha kukamilika kwa mradi huo katika ubora uliotakiwa na katika bajeti iliyopangwa mwaka 2012 bila kuongezeka pesa yoyote, kuanzia kitengo cha miradi ya PPF makao makuu, wabunifu na wasimamizi, mamlaka za Jiji, idara nyingine za Serikali na wakandarasi wenyewe.
Jengo hilo maalumu kwa shughuli za ofisi na biashara lenye ghorofa 10 sambamba na eneo la basmenet yenye uwezo wa kupaki magari 168, lina thamani ya shilingi bilioni 32.5. Limejengwa eneo la Corridor, Kitalu Na. 15 Barabara ya zamani ya Old Moshi Jijini Arusha. lina huduma zote muhimu kwa majengo ya kisasa zikiwemo 'lifti' za kutosha, majenereta makubwa, mataki ya maji na mafuta ya jenerato, mfumo wa kukabiliana na moto na bila kusahau camera 90 za usalama na eneo kubwa la kuegesha magari ndani ya jengo.
Kwa mujibu wa Mbunifu na Msimamizi Mkuu wa mradi huo wa kisasa, Arch Mawala, ujenzi wa jengo hilo ulianza rasmi Agosti 2 mwaka 2018 ukitarajiwa kukamilika miezi 104 baadae na ulikamilika rasmi (practica completion) mwishoni mwa mwezi Disemba mwakaa jana. Hata hivyo imewachukua miaka miwili na miezi 3 kuweza kukamilisha kila kitu katika ubora wa kiwango cha juu, ambapo miezi hiyo mitatu ni ya ngongeza ya muda kutokana na sababu ambazo hazikuweza kuzuilika.
Sehemu ya muonekano wa mbele wa jengo
Mpaka kufikia kukabidhiwa kwake hii leo, tayari ukaguzi wa mamlaka za Jiji na Usalama wa Majengo umeshakamilika na ruhusa ya matumizi kutolewa. Tayari jengo hilo limeshapata wapangaji watatu ambao wapo kwenye jengo tayari zikiwemo benki za TIB na FBNB, huku asilimia 21 ya wapangaji wengine wakiwa wamekwisha saini mikataba na PPF na wapangaji wengine 24 wakiwa katika mazungumzo.
Aidha kwa maelezo ya Mratibu wa PPF Kanda ya Kasakazini, Bw Onesmo Rushahi, Ofisi za Kanda ambazo kwa sasa ziko maeneo ya Kaloleni Jijini hapa zitahamishiwa katika Jengo hili jipya, huku mkakati wa PPF ukiwa ni kuhakikisha baada ya mwaka mmoja jengo hilo liwe limefanikiwa kupata wapangaji maeneo yote kwa shughuli za ofisi na biashara.
Mkandarasi Mkuu ni kampuni ya CRJE (EA) Ltd akisaidiwa na wakandarasi wengine kwa huduma za jengo kama vile ICT na Usalama - SSTL Group Ltd, Lifti - S.E.C (EA) Ltd, AC - M.A.K Enginering Co. Ltd, Mfumo wa maji safi na maji taka - Jandu Plumbers Ltd, na Umeme ni Central Electrical International Ltd. Pia kulikuwa na mamlaka za kiserikali kama wasimamizi wa usalama makazini OSHA, Idara ya maji Asurha - AUWSA, NAESCO, Halmashauri ya Jiji na Bodi za Ukaguzi kama AQRB na CRB.
Injinia Marko Kapinga, Meneja wa Utekelezaji wa Miradi ya PPF akikagua makabrasha yaliyokabidhiwa na mkandrasi kama michoro halisi ya namna jengo lilivyo kwa sasa
Kiongozi mkuu wa Kampuni ya CRJE (EA) Ltd, Bw Hu Bo (kulia) ambaye kamapuni yake ndio ilikuwa mkandarasi mkuu wa mradi akikabidhi funguo kwa Director General wa PPF Bw William Erio kama ishara ya makabdihiano ramsi ya jengo la PPF Plaza la Jijini Arusha hii leo. Kwa mbali anashuhudia Meneja wa jengo hilo kutoka PPF Bw..
Meneja wa PPF Uwekezaji Bw Selestine Some (kushoto) akimkabidhi ufungua kama ishara ya kuhamishia usimamizi wa jengo la PPF Plaza kwa Menenja Rasilimali, Bw Selemani Kituli wa PPF Kanda ya Kaskazini
Msimamizi Mkuu wa kazi zote za ujenzi kwa upande wa mkandarasi, kampuni ya CRJE, Bw Zhang Cuishan akitoa neno la shukrani katika hafla hiyo.
Director General wa PPF Bw William Erio kulia pamoja na mkuu wa uwekezaji (PPF's Director of Investiment) Bw Steven Alfred
DG William Erio katika picha ya pamoja mbeye ya sehemu kuu ya kuingilia kwenye jengo akiwa na timu ya wakandarasi, wasimamizi wabunifu wa mradi pamoja na wataalamu kutoka PPF Dar es Salaam.
Msanifu wa jengo na msimamizi mkuu wa mradi kutoka kampuni ya MD Consultancy Ltd, Arch Dudley Mawalla akiongoza ujumbe wa DG William Erio kufanya ziara ya ameneo mabalimabli ya jengo kabla ya makabidhiano rasmi.
Msafara ukitembelea eneo la kuegeshea magari chini ya jengo la PPF Plaza. Jumla ya magari 168 yanaweza kuegeshwa katika maeneo mbalimbali yaliyotengwa ndani ya jengo.
Director General William Erio akipata maelezo ya mfumo wa usalama wa kieletronic wa jengo namna unavyofanya kazi kutoka kwa mataalamu wa maswala ya usalama na mawasialiani ya kielectronic kutoka kampuni ya SSTL Ld, Bw Athumani Pongwe ndani ya chumba cha usalama. Jumla ya kamera 90 za usalama zimeunganishwa na taarifa zake kuletwa kwenye chumba hiki.
wakiangalia moja ya viambaza vya dani ya jengo.
Hapa DG William Erio na wataalamu wengine wakifurahia utani wa wake
Meeneja wa PPF Kaskazini Bw Onesmo Ruhasha, kulia na Director General wa PPF wakijadiliana jambo wakati wa kutembelea maeeneo ya jengo.
msimamizi mkaazi kwa niaba ya PPF, Injinia Norbert Nselu akimfafanulia DG Erio hatua kwa hatua namna ujenzi ulivyoanza mkapa kukamilika kwake.
Director General wa PPF akiangalia madhari ya Jiji la Arusha kutokea ghorofa ya nane katika moja ya baraza za jengo la PPF Plaza lililokamilika na kukabidhiwa hii leo. Pamoja nae ni Msanifu wa jengo na Msimamizi Mkuu wa Mradi Arch. D Mawalla
Bw Selemani Kituli (property manager wa PPF) na Bw Selestine Some, Meneja Uwekezaji wakifahamishana jambo katika hafla fupi ya makabidhiano ya jengo la PPF Plaza kutoka kwa Mkandarasi Mkuu CRJE (EA) Ltd
Sehemu ya timu ya washauri wasimamizi wa mradi kwa maswala ya gharama, uimara na huduma (Project Costs, Structural Strength na Building Services Engineering)
Mkuu wa Kampuni ya CRJE (EA) Ltd, kampuni ya kichina ambayo ndiyo ilikuwa mkandarasi mkuu wa mradi uliokamilika wa jengo la PPF Plaza la Jijini Arusha akitoa salamu zake katika hafla fupi ya makabidhiano ya jengo hilo
Director General wa PPF, Bw William Erio akisalimiana na Bi Getrude Haule, ambaye pia ni mmoja wa watumishi wa ofisi ya PPF Kanda ya Kaskazini iliyoko Kaloleni Jijini Arusha katika hafla ya makabidhiano ya jengo jipya la PPF Jijini hapa. Anayeshuhudia ni Bi Grace Estomih, mtumishi pia wa PPF Kanda ya Kaskazini ofisi ya Arusha.
Mbunifu/msanifu mkuu na msimamizi mkuu wa mradi wa jengo la PPF Plaza la Jijini Arusha, Arch. Dudley Mawalla akizungumza na wataalamu washauri wa masuala ya gharama za ujenzi ambao walisimamia fedha zote za mradi kwenda kwa wakandarasi na kuandaa bajeti yake, QS Mrosso (kushoto) kutoka kampuni ya Cost Consult Ltd ya Jijini Dar es Salaam.
PICHA&MAELEZO : TUMAINIEL SERIA, ARUSHA
No comments:
Post a Comment