Waziri
wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
akizungumza katika mkutano wa mwaka wa mapitio ya sekta ya afya
unaofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, wadau hao wa
Sekta ya afya wanajadiliana mambo mbalimbali na baada ya kumalizika kwa
mkutano huo kutakuwa na kusaini makubaliano yaliyofikiwa kwa
utekelezaji katika sekta ya afya hapa nchini , Katika picha kulia ni
Carol Hannon Mshauri wa Afya katika ubalozi wa Ireland nchini Tanzania.
Carol
Hannon Mshauri wa Afya katika ubalozi wa Ireland nchini Tanzania
akizungumza katika mkutano huo Kushoto ni Waziri wa Afya, Ustawi wa
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu.
Dk.Ulisubisya
Mpoki Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto akichangia hoja katika mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa
Karimjee jijini Dar es salaam.
Dk.
Deo Mtasiwa Naibu Katibu Mkuu wa Afya TAMISEMI akizungumza katika
mkutano huo ambao umekutanisha wadau wa afya na kujadili changamoto
mbalimbali zinazokabili sekta ya afya.
Baadhi ya wadau wakiwa katika mkutano huo
Waziri
wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
katikati na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Suleman Jafo wa
tatu kutoka kulia wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya
afya kwenye mkutano unaofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es
salaam.
Waziri
wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
katikati na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Suleman Jafo wa
tatu kutoka kulia wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya
afya kwenye mkutano unaofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es
salaam.
Mwaka
2015 Serikali ya Tanzania ilikamilisha Mpango wa Afya katika Jamii na
kuanzisha mafunzo kwa kada mpya za Wahudumu wa Afya ya Jamii (Community
Health Workers). Wafanyakazi hawa wana jukumu kubwa kuifikishia jamii
huduma za afya za msingi.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MPANGO
mkakati wa Sekta ya Afya wa Mwaka 2016 /2017 unahitaji sh.trioni 21
katika kuweza kutekeleza maeneo nane ya utoaji wa huduma kwa wananchi.
Akizungumza
na wadau wa afya leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema serikali itahakikisha
inakwenda sambasamba na mpango huo kutokana na kugusa kila sehemu
ikiwa ni lengo la kumfikia mwananchi wa kuweza kupata huduma ya afya.
Amesema
eneo mojawapo ni utoaji wa kinga ya afya kwa jamii pamoja na elimu juu
ya magonjwa kwa kuweka wataalam wenye mafunzo kutoka sehemu husika.
Ummy
amesema serikali imeanza kutoa mafunzo kwa wafanyakazi 4000 ambao
watafanya kazi na jamii moja kwa moja katika utoaji wa kinga ya afya
pamoja na elimu juu ya magonjwa mbalimbali.
Amesema
katika eneo la pili ni mgawanyo wa rasilimali fedha kwa kuhakikisha
kila kituo kinapata fedha na takwimu zake zitahifadhiwa juu ya fedha
wanazozipata kwa ajili ya dawa na vifaa tiba.
Waziri,
Ummy, amesema katika eneo la tatu ni juu ya uchangiaji wa huduma ya
afya bado ni changamoto hivyo katika mpango wanatarajia kupeleka mswaada
bungeni kwa kuwa na mfuko moja ambao kila mwananchi atachangia kwa
ajili ya huduma ya afya.
Aidha
amesema katika mpango huo wataangalia watumishi wa sekta ya afya kuwa
kila sehemu wanakuwepo katika kuweza kutoa huduma kwa wananchi ipasavyo
pamoja na masilahi ya motisha kwa watumishi walio pembezoni.
Waziri
Ummy amesema katika eneo lingine katika mkakati huo ni kuweka ufumbuzi
wa wa upatikanaji fedha na vyanzo vyake vikaeleka na uendeshaji pamoja
na rasilimali watu wanapatikana.
Amesema
sehemu ya nane ni utoaji wa nyota katika vituo vya afya ambavyo
vitapimwa kutokana na utoaji wake kwa kuanzia nyota ya kwanza hadi ya
nne.
Mkuruegenzi
Mtendaji wa Sikika, Irenei Kiria amesema hayo mambo yalikuwa
yakisubiliwa kwa muda mrefu na sasa serikali imeamua kuwajibika katika
utoaji wa huduma ya afya kwa wananchi wake.
Amesema
kuwa mpango mkakati ukienda kama ulivyopangwa jamii ya kitanzania
itaweza kupata huduma bora ya afya kutokana na mikakati iliyomo katika
mpango huo.
No comments:
Post a Comment