RAIA wa Japan, aliyejitambulisha kwa jian la Y.Miyaki, akiwa amejibandika tangazo kifuani, likielezea "Natafuta Daftari", huko Bombo barabara ya Tanga-Moshi. Miyaki ambaye amejibandika tangazo hilo, kifuani na mgongoni, aliibiwa vifaa vyake hapo Bombo akiwa kwenye basi moja "jina linahifadhiwa" akitoak Dar es Salaam kwenda mkoani Arusha. Miongoni mwa vitu alivyoibiwa nipamoja na laptop, camera na madaftari yake ya Research, yaani utafiti ambao ameufanya kwa takriban miezi sita (6) sasa.
Kijana huyo wa Kijapani ambaye ni mwanafunzi, anomba "Chonde chonde" wabongo walaosepa na vifaa vyake wafanye uungwana waalu daftari alipate maana limebeba mustakbal wa maisha yake yote. na ametangaza kutoa bahshishi ya shilingi 300,000 kwa atakayewezesha kupatikana kwa daftari lake hilo.
No comments:
Post a Comment