Dk 90+ 1: Yanga wanapata kona ya kwanza, lakini haina faida
Dk 87: Simba SC wanapata kona tena inazua kizaazaa langoni mwa Yanga kabla ya kuondoshwa kwenye hatari
Dk 82: Mashabiki wa Simba SC wanaanza kuachia siti zao Uwanja wa Taifa
Dk 80: Brian Majwega anakwedna kuchukua nafasi ya Ibrahim Hajib
Dk 72: Tambwe anaifungia Yanga bao la pili kwa guu la kulia akimalizia krosi ya Godfrey Mwashiuya kutoka kushoto
Amissi Tambwe anaifungia Yanga SC bao la pili Uwanja wa Taifa |
Dk 64: Godfrey Mwashiuya anakwenda kuchukua nafasi na Deus Kaseke
Dk 59: Danny Lyanga anachukua nafasi ya Hamisi Kiiza
Dk 52: Simon Msuva anachukua nafasi ya Haruna Niyonzima
Dk 46: Nova Lufunga anachukua nafasi ya Mwinyi Kazimoto
Dk 46: Kipindi cha pili kinaanza, Simba SC wanaukanyaga wakiwa pungufu baada ya Abdi Banda kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 25
Donald Ngoma ameifungia Yanga SC bao la kwanza Uwanja wa Taifa |
MPIRA NI MAPUMZIKO YANGA 1-0 SIMBA SC
Dk 45: Hassan Kessy anapiga mpira wa adhabu unapotea
Dk 44: Simba wanapata kona ya saba wanapoteza pia
Dk 44: Simba wanapata kona ya sita wanapoteza
Dk 39: Ngoma anaifungia Yanga bao la kwanza. Hassan Kessy alimrudishia pasi fupi kipa Vincent Angban, Ngoma akainasa akampga chenga kipa huyo na kufunga
Dk 35: Simba SC wanapata kona nyingine dakika ya 35, lakini inaokolewa
Dk 25: Abdi Banda anaonyeshwa kadi ya njano ya pili na kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu tena Ngoma
Refa Jonesia Rukyaa akimuonyesha kadi nyekundu Abdi Banda wa Simba SC |
Dk 20: Barthez ameinuka na mchezo unaendelea
Dk 18: Simba wanapiga kona nyingine, Barthez anacheza anaanguka na kupatiwa huduma ya kwanza
Dk 17: Simba wanapata kona ya tatu inazaa kona nyingine
Dk 14: Simba wanapata kona ya pili haina faida
Dk 8: Simba wanapata kona ya kwanza, lakini haina faida
Dk 1: Juuko anamchezea rafu Ngoma mpira unapigwa kwenda Simba
Saa 10:00: Mpira umeanza, wameanza Yanga
Saa 9:53: Timu ndiyo zinaingia uwanjani sasa
Saa 9:40: Timu zimemaliza kupasha misuli moto na zimerudi vyumbani tayari kuingia uwanjani tena kuanza mchezo
Vikosi;
Yanga SC: Barthez, Abdul, Bossou, Twite, Mngwali, Ngonyani, Kaseke, Kamusoko, Tambwe, Ngoma na Niyonzima.
Simba SC: Angban, Kessy, Tshabalala, Juuko, Banda, Majabvi, Mkude, Kazimoto, Kiiza, Hajib na Ndemla
No comments:
Post a Comment