Pages

February 6, 2016

JK AONGOZA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 39 YA CCM MKOANI SINGIDA LEO


 Shamra shamra kutoka kwa bendi ya Tot Plus ikinogesha sherehe hizo
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi waliokuwa wamekusanyika kwenye uwanja wa Namfua kushuhudia sherehe za maadhimisho ya miaka 39 ya CCM mapema leo mchana mkoani Singida
 Rais John Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete
 Rais John Magufuli akimpongeza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa hotuba yake wakati wa maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa CCM Namfua, mjini Singida leo. 
 Mwenyekiti wa CCM,Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt  Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wakazi wa Singida na vitongoji vyake ndani ya uwanja wa namfua,wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM,mkoani Singida
 Wageni waalikwa mbalimbali walikuwepo wakiwemo wasani wa bongo muvi  

 Sehemu ya umati wa wananchi wakiwa katika maadhimisho hayo.
 Baadhi ya Wananchi na wafuasi wa chama cha Mapinduzi (CCM) wakisikiliza hotuba iliyokuwa ikisomwa na Mwenyeki wa chama hicho,Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 39 tangu kuanzishwa kwake ndani ya uwanja wa Namfua leo mchana mkoani Singida.
 Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Kikwete akiwa ameongozana na Rais Dkt John Pombe Magufuli wakishuka jukwaani kwa pamoja mara baada kuhitimisha shughuli za maadhimisho ya miaka 39 ya chama hicho mkoani Singida,nyuma ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluh Hassan.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Rais Dkt John Pombe Magufuli
 Rais John Magufuli akiwasalimia wananchi baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa CCM Namfua, katika maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM ambayo kitaifa yamefanyika leo mkoani Singida. Kutoka kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana.
 Rais Magufuli akiwapungia mkono wananchi.
 Rais Magufuli akisalimiana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akijadiliana jambo na Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu pamoja na Nape Nnauye.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais mstaafu Jakaya Kikwete akilakiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Kinana alipowasili kwenye Uwanja wa CCM Namfua, mjini singida kuongoza maadhimisho ya miaka 39 ya CCM.
 Rais John Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM, UJakaya Kikwete
 JK akisalimiana na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan. Katikati ni Rais Magufuli.
 Mtoto Yusufu anayeandaliwa na babake kuwania urais 2050 akiwa kwenye baiskeli aliyotengenezewa na babake pichani.
 Mwanamuziki wa Bendi ya Yamoto Band akiwaimbisha wananchi wakati wa sherehe hizo.
 Bendi ya Yamoto ikitumbuiza wakati wa maadhimisho ya miaka 39 ya ccm kwenye Uwanja wa Namfua, Singida.
 Kikundi cha TOT kikitumbiza kwa wimbo maalumu wa maadhimisho ya miaka 39 ya CCM
 Watoto wakipiga mafataki kunogesha maashimisho hayo
 Rais Magufuli akimpongeza aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mashishanga kujiunga na CCM akitokea Chadema.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Cresto Haja aliihama Chadema na kujiunga na CCM
 Rais John Magufuli akimpongeza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa hotuba yake wakati wa maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM, wakati wa maadhimisho yhayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa CCM Namfua, mjini Singida leo. Kutoka kushoto ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete na Samia Suluhu Hassan Makamu wa Rais.
Sehemu ya umati wa wananchi wakiwa katika maadhimisho hayo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...