Pages

February 3, 2016

HATUWEZI KUFANYA MABADILIKO KWA MASHINIKIZO-TANZANIA


Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, akichangia majadiliano ya Bodi ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto ( UNICEF) hapo siku ya jummane. Katika mchango wake, Balozi amewaeleza wakuu wa UNICEF kwamba, mabadiliko ya kweli yanayolenga kuboresha hali bora ya maisha ya makundi yote ya jamii, wakiwamo watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali hayawezi kufanyika kwa mashinikizo kutoka nje bali yatafanyika kwa ushiriano na ubia wa dhati baina ya Serikali, Wadau waMaendeleo na Wananchi wenyewe. Vile vile Balozi Manongi akasisitiza kwamba UNICEF inapashwa kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia bajeti iliyojipangia badala ya kutegemea misaada kutoka kwa wahisani, hususani Asasi zisizo za kiserikali kwa kile alichosema, mara nyingi Asasi hizo hutoa misaada yao kwa malengo ya kushinikiza ajenda zao na maslahi binafsi,

Mkutano huo pia ulipokea na kupitisha mpango kazi wa utekelezaji wa miradi ya UNICEF pamoja na rasimu ya Ripoti ya Tanzania ambayo imeainisha masuala mbalimbali pamoja na miradi ya maendeleo inayorajiwa kutekelezwa na UNICEF kwa Tanzania. Aliyeketi na Balozi ni Afisa wa Uwakilishi Bi.Ellen Maduhu
Meza kuu ya Wakurugenzi na Watendaji wa UNICEF wakati wa mkutano wa Bodi hiyo uliofanyika siku ya jumanne na kuhudhuriwa na wajumbe wa Bodi hawapo picha pamoja na wajumbe wengine waalikwa. Tanzania ilialikwa katika mkutano huo kama msikilizaji.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...