Pages

February 1, 2016

Cristiano Ronaldo apiga hat-trick dhidi ya Espanyol, haya ndio matokeo kamili

Ligi Kuu Hispania imeendelea  January 31 kwa michezo kadhaa kuchezwa nchiniHispania, klabu ya Real Madrid ya Hispania ilikuwa katika dimba lake la Santiago Bernabeu kuwakabili EspanyolReal Madrid ambao wapo nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Hispania waliingia dimbani kuhakisha hawapotezi wala kuacha point hata moja ili waweze kuwa na nafasi nzuri ya kuwaombea FC Barcelona naAtletico Madrid wafanye vibaya.
1454274308785_lc_galleryImage_Real_Madrid_s_French_forw
Real Madrid wakiwa chini ya kocha wao Zidane wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 6-0 dhidi ya Espanyol na kutimiza jumla ya point 47 huku wakiwa nafasi ya tatu kwa tofauti ya pont nne na wapinzani wao FC Barcelona wanaoongoza Ligi lakini wapo nyuma mchezo mmoja.
1454270008809_lc_galleryImage_Real_Madrid_s_Karim_Benze
Kikosi cha Zidane ambacho safu yake ya ushambuliaji iliongonzwa na Cristiano Ronaldoambaye kafunga hat-trick, walianza kupata goli la kwanza dakika ya 7 kupitia kwa Karim Benzema, baadae Cristiano Ronaldo aliyefunga goli la pili dakika ya 12 na baadae akafunga magoli mengine mawili dakika ya 45 na 82, baada ya James Rodriguezkufunga goli la tatu dakika ya 16, goli la sita Espanyol walijifunga wenyewe dakika ya 87 kupitia kwa Oscar Duarte.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...