Pages

December 16, 2015

MKUU WA MKOA WA ARUSHA AKIFUNGIA KIWANDA CHA SARUJI


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda  amekifungia kiwanda cha Saruji kinachofahamika kwa jina la Arusha Zaidi Cement Company kilichopo eneo la Ngaramtoni jijini Arusha   kutokana na uendeshaji wa kiwanda hicho kugubikwa na utata kuanzia kwenye uzalishaji,wamiliki na mazingira kutokuwa na usalama kwa wafanyakazi wake.

Mkuu huyo wa Mkoa amefanya ziara ya kushtukiza akiambatana na maafisa wa Mamlaka ya Ukusanyaji wa Mapato TRA ndipo alipobaini kuwa kiwanda hicho kimekua kikikwepa kulipa kodi hivyo kukifunga kwa muda usiojulikana.


Mkuu  wa mkoa wa Arusha, Daudi Felix Ntibenda akitazama Kontena lililosombwa na mafuriko kutoka ng`ambo ya barabara hadi katikati ya barabara jana katika eneo la Ngaramtoni kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha  na kusababisha madhara mbalimbali .


Aidha amemtaka mmiliki wa kiwanda hicho ambaye hakufahamika mara moja kuhakikisha kuwa anafika kwenye Ofisi za mkuu wa mkoa kutoa taarifa ya kiwanda hicho pia ameuagiza uongozi wa mkoa kwa kushirikiana na Wataalamu kufanya tathmini ya mazingira kwani kiwanda hicho kinachangia uharibifu wa mazingira.

‘Ukiuliza mmiliki wa kiwanda hiki ni kigugumizi haeleweki,mazingira haya si salama na uendeshwaji wa shughuli za hapa bado una utata hivyo naagiza kiwanda hiki kifungwe mara moja na wafanyakazi wote waende majumbani” Alisema Ntibenda

Amemtaka Mmiliki wa Kiwanda hicho kufika katika Ofisi zake na kutoa maelezo yanayohitajika pamoja na kuimarisha ulinzi katika kiwanda hicho .


Moja kati ya Viongozi wa kiwanda hicho ambaye hakufahamika jina lake mara moja amekanusha na kudai kuwa wamekua wakilipa kodi kwa serikali huku akikataa kuzungumza na waandishi juu ya wamiliki wa kiwanda hicho

Tanzania imekua ikikabiliwa na tatizo la viwanda bubu  ambavyo vimekua vikizalisha bidhaa zinazoathiri afya za binadamu na kukiuka sheria na taratibu za nchi ,hivyo viongozi wa serikali na mamlaka husika hazina budi kuchukua hatua stahiki ili kunusuru afya na maisha ya Watanzania.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...