Pages

December 19, 2015

Baada ya kumtimua Jose Mourinho, Chelsea imetangaza kocha wa muda wa timu yao ….

Uongozi wa klabu ya Chelsea December 16 iliripotiwa kuweka kikao cha dharura kujadili mwenendo wa timu yao kwa sasa, Chelsea baada ya kukaa kikao hicho cha bodi, December 17 walitangaza rasmi kumfuta kazi Jose Mourinho na nafasi yake kubaki wazi.
Stori mpya ni kuwa uongozi wa klabu ya Chelsea December 19 umetangaza rasmi kumteua kwa mara ya pili Guus Hiddink kuwa kocha wa muda wa kukinoa kikosi.Chelsea imemfukuza Mourinho baada ya kuiongoza kucheza mechi 16 za Ligi KuuUingereza msimu huu, kufungwa tisa, sare mitatu na kushinda minne.
guus_hiddink_1295965c
Hii sio mara ya kwanza kwa Chelsea kumteua Guus Hiddink kuwa kocha wa muda wa klabu hiyo, lakini sio mara kwanza kwa Chelsea kumfukuza Jose Mourinho. Kwa mara ya kwanza Chelsea ilimteua Guus Hiddink kuwa kocha wa muda mwaka 2009, lakini kwa upande wa Mourinho kwa mara ya kwanza alifutwa kazi akiwa na Chelsea mwaka 2007

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...