Pages

October 5, 2015

UNESCO YAWAKUTANISHA VIONGOZI WA DINI,MILA NA REDIO ZA JAMII KUHAMASISHA AMANI KATIKA UCHAGUZI

Katibu Mkuu wa Baraza la Mahedhebu kwaajili ya Amani,Mchungaji,Canon Thomas Godda akizungumza katika kongamano la Amani lililoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,Sayansi na Utamaduni(Unesco)kwa kushirikiana na madhehebu ya Dini na Viongozi wa Mila ili kuhamasisha amani katika kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi.

Mwenyekiti wa Radio za Jamii kutoka Unesco na Mhadhiri Mwandamizi wa Mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Hyderabad,Profesa Vinod Pavarala akizungumza katika kongamano la amani,wanaofatilia kwa karibu ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Dini kwaajili ya Amani,Mchungaji Thomas Godda na Afisa Miradi wa Unesco,Al-Amin Yusuph.

Mjumbe wa Bodi ya Muungano wa Redio za Jamii nchini(COMNETA)Balozi Christopher Liundi akichangia mada ya umuhimu wa matumizi ya Redio za Jamii.

Kiongozi wa Mila ya jamii ya wafugaji katika Kijiji cha Terrat wilaya Simanjiro mkoa wa Manyara,Lesira Samburi akizungumza kwenye kongamano la kuhamasisha amani kuelekea uchaguzi Mkuu.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Redio ya Jamii 94.9 Mkoani,Pemba,Hamdu Hasan Bakari(kushoto)akiteta jambo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Dini kwaajili ya Amani,Mchungaji Thomas Godda

Katibu Mtendaji wa Baraza la Dini kwaajili ya Amani,Mchungaji Thomas Godda(kushoto)akiteta jambo na maafisa wa Unesco,Nancy Kaizirege na Al -Amin Yusuph

Ujumbe wa Muungano wa Redio za Jamii,Wazee wa Mila na Viongozi wa dini wakiwasili kwenye kiwanda cha kuzalisha nishati kwanjia ya Mibono katika Kijiji cha Terrat ambacho kimekua msaada kwa wananchi wengi.

Ujumbe wa Muungano wa Redio za Jamii,Wazee wa Mila na Viongozi wa dini wakiwasili kwenye kiwanda cha kuzalisha nishati kwanjia ya Mibono katika Kijiji cha Terrat ambacho kimekua msaada kwa wananchi wengi.

Mbegu zinazotumika kuzalisha mafuta kwaajili ya nishati


Afisa Miradi wa Unesco,Al-Amin Yusuph akivishwa mavazi ya jamii ya wafugaji wa kimaasai ikiwa ni ishara ya kumpongeza na kumuaga baada kuhamishwa kikazi nchini India,kushoto ni Mwenyekiti wa Muungano wa Redio za Jamii nchini(COMNETA)Joseph Sekiku.

Viongozi wa Mila wakionesha ujumbe wa kuhamasisha amani .

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...