Kuna Tuzo zinaitwa ANZISHA AWARDS, nimezifahamu leo baada ya kukuta kuna majina wa Watanzania wawili ambao wametajwa kwenye vijana 12 waliotajwa kuwania Tuzo hizo mwaka 2015.
Tuzo hizo zimeanzishwa kwa ajili ya kuwatambua na kuwatuza Vijana wenye umri wa kati ya miaka 17 na 22 ambao wanajihusisha na ujasiriamali na kupitia ujasiriamali wao wamesaidia kubuni miradi ambayo inatatua baadhi ya changamoto za Kijamii.
Kwenye majina ya Vijana 12 waliotajwa kuwania Tuzo hizo wako pia Watanzania wawili,George Mtemahanji mwenye umri wa miaka 22 na Sirjeff Dennis ambaye ana miaka 21.
Vijana wote 12 hawa hapa.
Huyu ni George Mtemahanji, Mtanzania ambaye ameingia kwenye Tuzo hizo baada ya kuanzisha mradi wa umeme wa Jua na Kampuni yake inaitwa SunSweat Solar Limited, Kampuni yake inahudumia watu waishio Vijijini ambako kuna tatizo kubwa la umeme.
Mtanzania mwingine ni huyu, Sirjeff Dennis… yeye nae yumo, Mradi alioanzisha ni wa kukabiliana na Changamoto ya ukosefu wa Chakula pamoja na umaskini Vijijini, kupitia ufugaji wa Kuku na Kilimo cha mbogamboga. Jamaa pia ana Kampuni yake ambayo kaipa jina la Jefren Agrifriend Solutions, Biashara yake kubwa ni kuuza Kuku na Mayai.
Fabrice Alomo, kijana wa Cameroon ambaye ameanzisha Website yaMyAConnect ambayo inasaidia Wafanyabishara wadogowadogo kuuza bidhaa kwa njia ya Mtandao.
Mabel Suglo, huyu ni kijana wa Ghana ambaye naye ameingia kwenye list ya vijana hao 12, yeye aliguswa na nafasi ya watu wenye ulemavu kwenye Jamii.. akaona aanzishe kitu kinaitwa Eco-Shoes Project ambapo aliowaajiri kufanya kazi ya kutengeneza viatu ni watu wenye ulemavu… Viatu vinatengenezwa kwa Matairi na nguo ambazo zimechakaa na hazifai kuvaliwa.
Vanessa Zommi… huyu mrembo anatoka Cameroon na umri wake ni miaka 19 tu, lakini alianzisha Kampuni ya Emerald Moringa Tea, ambayo inatengeneza majani ya Chai yanayosaidia kufanya mfumo wa Chakula mwilini kuwa vizuri, unaambiwa majani anayotengeneza ni ya kutokana na mmea ambao Cameroon wanauita Moringa.
Huyu ni Mnigeria, Chris Kwekowe ambaye alianzisha System ya kujisomea Mtandaoni ambayo inaitwa Slatecube na kusaidia hata wasio na uwezo wa kulipia gharama za Vyuo kujisomea Mitandaoni kwa urahisi kabisa.
Daniel Mukisa kutoka Uganda. Daniel bado ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Makerere, ameanzisha mradi wa Usafirishaji kwa kutumia Baiskeli, aliona kuna ishu ya foleni na pia Barabara mbovu kwenye maeneo mengi, mradi wake unalenga kufikisha bidhaa mpaka nyumbani kwa wateja ambao wamenunua bidhaa kwa njia ya Mtandao, kwa baiskeli bidhaa zinawafikia wateja kwa haraka na inasaidia pia kuokoa gharama za usafirishaji.
Chantal Butare, mrembo mwingine kutoka Rwanda ambaye alianzishaKinazi Dairy Cooperative, mradi ambao unawasaidia Wafugaji wadogowadogo 3,200 kuuza maziwa ya ng’ombe wao. Soko la maziwa hayo liko ndani ya Rwanda na Burundi na kazi ya kuuza inasimamiwa na huyu mrembo.
Karidas Tshintsholo kutoka South Africa… nae yumo kwenye Washiriki 12 waliopita kuingia kwenye Tuzo hizo, yeye ana mradi wa Push Imsokol Clothing ambapo anajihusisha na kutengeneza T-shirt, Kofia na Masweta ambayo yana soko zuri ndani ya South Africa.
No comments:
Post a Comment