Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza mbele ya Mabalazi na Wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Wizara kwa ajili ya kumuaga rasmi Balozi wa Hispania aliyemaliza muda wa kazi nchini, Mhe. Luis Manuel Cuesta Civis. Katika hotuba yake Mhe. Membe alimshukuru Balozi Luis kwa mchango wake wa kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Hispania. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Agosti, 2015. |
No comments:
Post a Comment