KOCHA wa Mpito wa
Timu ya taifa Taifa Star, Mzawa kutoka Uluguruni, Charles
Boniface Mkwasa ‘Master’ (pichani kulia na msaidizi wake) ametangaza kikosi cha wachezaji 26 wanaoingia
kambini
jijini Dar es Salaam kesho kujinoa na mashindano ya kimatafa.
Mkwasa akiwa ameongozana na
Msaidizi wake Hemed Morocco mapema alisema kikubwa wanachofanya sasa ni kurudisha
imani ya watanzania juu ya timu yao ya Taifa, kisha watajitahidi kadri ya uwezo
wao kuhakikisha kuwa timu inafanya vizuri katika michezo inayowakabili.
Aidha Mkwasa ametangaza benchi la ufundi la timu ya Taifa ambalo litakuwa na kocha msaidizi Hemed Morocco, kocha wa magolikipa Peter Manyika, Mshauri wa timu Abdallah Kibadeni, mtunza vifaa Hussein Swedi Gaga huku mratibu wa timu akiwa ni Alhaj Ahemd Mgoyi.
Wachezaji 26 watakaoingia
kambini kesho alhamisi katika hoteli ya Tansoma tayari kwa ajili ya maandalizi
ya mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda ni pamoja na makipa: Mudathir Khamis (KMKM), Mwadini Ally
(Azam), Ally Mustafa “Barthez” (Yanga).
Walinzi: Shomari Kapombe (Azam), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Mohamed Hussein “Tshabalala” (Simba), Haji Mwinyi (KMKM), Nadir Haroub “Cannavaro” (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Hassan Isihaka (Simba), Aggrey Morris (Azam).
Walinzi: Shomari Kapombe (Azam), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Mohamed Hussein “Tshabalala” (Simba), Haji Mwinyi (KMKM), Nadir Haroub “Cannavaro” (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Hassan Isihaka (Simba), Aggrey Morris (Azam).
Viungo: Jonas Mkude (Simba),
Abdi Banda (Simba), Salum Telela (Yanga), Frank Domayo (Azam).
Viungo wa pembeni: Saimon
Msuva (Yanga), Said Ndemla (Simba), Deus Kaseke (Mbeya City), Ramadhan Singano
“Messi” (Simba).
Washambuliaji: John Bocco (Azam), Atupele Green (Kagera Sugar), Rashid Mandawa (Kagera Sugar) na Ame Ally (Mtibwa Sugar).
Wachezaji Juma Abdul (Yanga), Mudathir Yahya (Azam) na Samwel Kamuntu (JKT Ruvu) wameitwa kama wachezaji wa akiba katika kikosi cha timu ya Taifa kinachoingia kambini kesho.
No comments:
Post a Comment