KAMPUNI
ya ACACIA inayojishughulisha na uchimbaji na utafutaji madini,
imezindua kampeni ya kukusanya fedha kupitia kupanda mlima Kilimanjaro,
leo Jumatatu Juni 22, 2015, ambapo fedha hizo zitakwenda kusaidia sekta
ya elimu kwenye maeneo yanayozunguka migodi mitatu inayomilikiwa na
kampouni hiyo ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi.
Akizungumza
muda mfupi kabla ya kuanza kwa safari ya kupanda mlima Kilimanjaro
kwenye lango la Machame,iliyo shirikisha watu 21, Afisa Mtendaji Mkuu wa
kampuni hiyo, Brad Gordon, alisema, kampuni yake ilianzisha mpango
ujulkikanao kama “CAN EDUCATE”, ikimaanisha tunaweza kujieleimisha,
imeamua kukusanya fedha kupitia kupanda mlima Kilimanjaro, ili kusaidia
elimu na kampuni inimekuwa ikifanya hivyo kila mwaka.
“Lengo
ni kukusanya dola za Kimarekani 200,000, zitakazosaidia jamii inayokaa
kuzunguka maeneo ya migodi inayomilikiwa na kampuni hiyo” alisema Meneja
Mkuu wa Uendelezaji wa Kmapuni, Asa Mwaipopo.
Na
kuongeza kuwa kuna watoto wengi wanashindwa kendelea na elimu ya
sekondari na ile ya chuo kikuu, sio kwa sababu za uwezo mdogo wa
kimasomo, bali ni ukosefu wa fedha za kuendelea na elimu.
Acacia imeamua kushiriki katika kuwasaidia watoto hawa ili watimize ndoto zao. Alimaliza Mwaipopo. Pichani, Afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya ACACIA, Brad Gordon, (Wapili kushoto), akiongoza timu ya watu 21 wakiwemo wafanyakazi, marafiki na familia za wafanyakazi wa kampuni hiyo ,kupanda Mlima Kilimanjaro kwenye lango la Machame mkoani Kilimajaro Jumatatu Juni 22, 2015, kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu nchini.(Habari na K-VIS MEDIA, picha na Dixon Busagaga)

Kundi
la watu 21, wakiwemo, wafanyakazi wa Acacia na familia zao pamoja na
marafiki wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza safari yao ya
kupanda Mlima Kilimanjaro Juni 22, 2015
Afisa
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Acacia, Brad Gordon, (katikati), akiwa na
Meneja Mkuu wa Uendelezaji wa kampuni hiyo, Asa Mwaipopo, (kushoto),
akizungumza muda mfupi kabla ya kuongoza timu ya wapanda mlima
Kilimanjaro kwa nia ya kukjsuanya fedha hizo
Brad, (kushoto), akijadiliana jambo na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Necta Pendaeli Foya (katikati)
No comments:
Post a Comment