Waziri Mkuu, Mizengo Peter Pinda ameunda kamati maalumu ya kudumu ya kusimamia Usafiri wa barabarani nchini ili kutatua changamoto zinazoikabali sekta ya Usafiri.
Katika
kamati hiyo mwenyekiti wake atakuwa katibu mkuu wa wizara ya chukuzi,
Katibu akiwa kamishna wa polisi barabarani na Mkurugenzi wa SUMATRA huku
wajumbe wakiwa ni pamoja na katibu mkuu wizara ya kazi ya na ajira,
katibu mkuu ujenzi, mwanasheria mkuu wa serikali na naibu katibu mkuu
ofisi ya waziri mkuu.
Mkuu
wa ratibu wa idara ya maafa toka ofisi ya waziri mkuu, mwenyekiti wa
TABOA na TATOA, CHAKUA nao wanatakiwa kuanza kufanya vikao leo na kila
mwezi watakutana kujadili na kutatua changamoto zote kasoro zile za
kisheria ambazo zitapelekwa serikalini kwa mchakato zaidi wa
kuzirekebisha.
Wakati
huo huo umoja wa vyama vya madereva nchini Tanzania umesema hauna
taarifa juu ya wao kutakiwa kukutana na waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda
kwa ajili ya mazungumzo kama inavyozungumzwa na kusisitiza kuwa wao
wataendelea na mgomo wao ulioanza leo mpaka masuala yao yatapofanyiwa
kazi.
Akizungumza
na East Africa Radio leo Makamu Mwenyekiti wa Muungano wa vyama vya
Madereva Abdallah Lubala amesema kauli ya kuwa wamekubaliana kukutana na
Mh. Pinda ni za kisiasa na hazina ukweli wowote hivyo wataendelea na
mgomo wao.
Wakati
huo huo mgomo huo ambao umetangazwa kwa nchi nzima athari zake
zimejitokeza katika mikoa mingine tofauti ambapo madereva wa mabasi ya
abiria wamegoma huku wasafiri wakitumia usafiri mbadala wa bajaji pamoja
bodaboda.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa jiji la Mbeya, Arusha na Mwanza
wamesema kuwa wanalazimika kutembea umbali mrefu kwenda makazini na
wangine wakitumia gharama kubwa kutokana na vyombo hivyo wanavyotumia
kupandisha bei za nauli kuliko kawaida.
Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment