Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (wa pili kulia), Balozi wa
China nchini, Mh. LU Youqing (kushoto), Afisa utawala na fedha wa
UNESCO, Spencer Bokosha (kulia), Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu
Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmar pamoja na mkalimani wa Balozi wa China
wakifurahi jambo wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Profesa Sifuni Mchome (hayupo pichani) akiwasili kwenye chumba
cha mikutano Wizara ya Elimu kwa ajili ya hafla fupi ya kutiliana saini
mkataba utakaowezesha kutekelezwa kwa mradi wa kuwezesha walimu wa
Tehama vyuoni nchini. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Modewji blog team
SERIKALI
na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) jana wametiliana saini mkataba utakaowezesha kutekelezwa kwa
mradi wa kuwezesha walimu wa Tehama vyuoni nchini.
Akizungumza
baada ya kutiwa saini kwa mkataba huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome alisema mradi huo ni mkombozi
mkubwa katika maandalizi ya kufundisha kwa kutumia Tehama nchini.
Alisema
mpango huo wenye kuwezesha walimu kujifunza Tehama unafadhiliwa na
Serikali ya Jamhuri ya watu wa China ambao ndio wamepitisha fedha zao
UNESCO.
Katika
utiaji saini huo ambapo Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing
alikuwepo, katika jumla ya uhai wa mradi ambao ni miaka miwili ,
miundombinu ya ufundishaji masomo ya sayansi na hesabu katika vyuo vya
walimu vya Monduli na Tabora itaboreshwa.
Katika mradi huo walimu watafundishwa elimu ya Tehama, namna ya kufundisha na kujifunza.
Katibu
mkuu Mchome alisema kwamba vyuo hivyo viwili vitawezeshwa kuwa na
mtandao ambao utaunganishwa na vyuo vingine vinane vya masomo ya sayansi
na hesabu kwa ajili ya kubadilishana taaluma.
Pia
vyuo hivyo vitawezeshwa kuandaa programu zenye kuelezea mfumo wa utoaji
huduma za Tehama kwa ajili ya walimu wa masomo ya sayansi na hesabu.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (katikati) akisalimina kwa
furaha na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa
Sifuni Mchome (kulia) na kushoto ni Balozi wa China nchini, Mh. LU
Youqing (aliyeipa mgongo kamera).
Profesa
Mchome alisema ili taifa liweze kusonga mbele katika mpango wake wa
kufundisha kwa kutumia Tehama ni vyema kuandaa walimu na fedha za China
kupitia Unesco zitasaidia maandalizi hayo.
“Tunaamini
tukiwekeza katika vifaa vya kupromoti Tehama, walimu wakifundishwa na
kuandaliwa vyema, wataenda kusaidia kufundisha na kuwezesha matumizi ya
Tehama katika shule zao.” Alisema Profesa Mchome.
Alisema japo zipo program ndogo nyingine , program waliyotia saini jana
ilikuwa kubwa na yenye tija itakayoimarisha ubora wa elimu kwa kuwapa
wanafunzi elimu ya kujitegemea, elimu yenye kuwakwamua kiujuzi na
kuutumia ujuzi huo kwa maendeleo yao na taifa.
Tanzania
ni miongoni mwa mataifa barani Afrika ambayo mapema wametambua thamani
ya kufundisha kwa njia ya Tehama ili kuboresha elimu na mfumo wa elimu.
Taasisi
zitakazohusika na mradi huo ni pamoja na Chuo Kikuu Huria (OUT) na
Taasisi ya Elimu nchini(TIE) kwa kuratibiwa na Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome
(kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira
Rodrigues (katikati) pamoja na Balozi wa China nchini, Mh. LU Youqing
(kushoto) kabla ya kutiliana saini mkataba huo.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza jambo kabla ya
kusaini mkataba huo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome na Kulia ni Kaimu Katibu
Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dr. Moshi Kimizi. Waliosimama
wakishuhudia tukio hilo kutoka kushoto ni Joel Nanauka wa UNESCO, Afisa
tawala msaidizi wa UNESCO, Rahma Islem, Afisa mipango wa utamaduni wa
UNESCO, Rehema Sudi, Balozi wa China nchini, Mh. LU Youqing, Ofisa
anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmar pamoja
na Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome wakitiliana
saini mkataba utakaowezesha kutekelezwa kwa mradi wa kuwezesha walimu wa
Tehama vyuoni nchini unaofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya watu wa
China. Wanaoshuhudia tukio hilo waliosimama ni Balozi wa China nchini
Tanzania, Mh. LU Youqing (wa pili kushoto), Ofisa anayeshughulikia
masuala ya elimu kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmar (wa pili kulia), Afisa
mipango wa utamaduni wa UNESCO, Rehema Sudi (kushoto), Afisa utawala na
fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha na Kulia aliyeketi ni Kaimu Katibu
Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dr. Moshi Kimizi.
Zoezi la kusaini mkataba likiendelea.
Wakifurahi kwa pamoja mara baada ya zoezi la kutia saini kukamilika.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome
wakibadilishana hati za mkataba utakaowezesha kutekelezwa kwa mradi wa
kuwezesha walimu wa Tehama vyuoni nchini unaofadhiliwa na Serikali ya
Jamhuri ya watu wa China. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Balozi wa China
nchini Tanzania, Mh. LU Youqing(wa pili kushoto) pamoja na Afisa utawala
na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha (kulia).
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza jambo
baada ya kutiliana saini mkataba huo.
Afisa
utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha (kulia) akizungumza jambo
na Afisa wa ubalozi wa China (katikati) na Kushoto ni Afisa Utawala
msaidizi wa UNESCO, Rahma Islem.
No comments:
Post a Comment