Toka kushoto ni Kathrin Hoff, kijana Paulo, Masoud Kipanya na Balozi Henry Mdimu.
Taasisi
ya Imetosha ya jijini Dar es Salaam leo hii imepeleka misaada mbali
mbali katika kijiji cha watoto wasioona cha Buhangija, mkoani Shinyanga
ambacho kwa sasa kinahifadhi pia watoto na vijana wenye ualbino takriban
300.
Misaada
hiyo ikiwemo mabelo ya mitumba 2 moja la masweta na jingine la suruali
za jeans, unga, mchele, maharage, sukari, chumvi, ndoo 3 za mafuta ya
kupikia, sabuni za kufulia box 8, vile vile box 3 za vifaa vya hedhi
vitakavyodumu miezi miwili pamoja na nguo za ndani dazeni 12 vyote hivo
imegharimu Tsh milioni mbili na elfu sitini(2,060,000) ambazo
zimetolewa na wanachama wa taasisi hiyo iliyojikita kupambana na mauaji
ya watu wenye ualbino kwa njia ya elimu.
Akiongea na watoto na vijana hao Mwenyekiti Masoud Kipanya alisema
taasisi hiyo inaangalia jinsi ya kutengeneza mazingira kwa kituo hicho
kujijengea uwezo wa kujipatia chakula badala ya kutegemea wasamaria wema
huja pale watakapojisikia wakati watoto katika kituo hicho wanahitaji
kula kila siku.
Mkuu wa kituo hicho aliishukuru taasisi ya Imetosha kwa kuonesha mapenzi
ya dhati na watoto wa kituo hicho na kuguswa na changamoto
zinazowakuta, kwani si mara nyingi sana watu au taasisi kurudia kupeleka
misaada kituoni hapo kitu ambacho Imetosha wamekifanya. Wiki 3
zilizopita taasisi hiyo ilipeleka msaada wa chakula kituoni hapo.
Awali mtafiti wa masuala yahusuyo watu wenye ualbino mJerumani
Bi Kathrin Hoff alielezwa kufurahishwa na jitihada zinazooneshwa na
Imetosha kwa uhamasishaji inayoufanya kwa jamii ya Ki Tanzania, pia
amepongeza sana hatua ya Imetosha kutaka kukifanya kituo cha Buhangija
kujitegemea badala ya kubaki tegemezi kama ilivyo sasa. Kathrin Hoff ni
mhitimu toka chuo kikuu cha Mainz nchini Ujerumani.
|
Baadhi ya missada iliyotolewa na Imetosha pembeni kulia ni mabelo mawili ya mguo. |
Mkuu wa kituo hicho Bw Peter Ajali akiongea na watoto wa kituo hicho akieleza dhamira ya ya asasi ya Imetosha kwao. |
Hapa wakimsikiliza Masoud Kipanya |
Baadhi ya wasichana wa kituoni hapo wakifurahia msaada wa nguo za ndani na vifaa vya hedhi walivyokabidhiwa na mjumbe wa Imetosha aishiye Shinyanga Bibi Herriet |
Picha na habari kwa hisani ya Tanzania
Bloggers Network kanda ya kati.
No comments:
Post a Comment