Meneja
wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza
Bw. Felician Ncheye akiwakaribisha mameneja wa Redio za jamii nchini
(hawapo pichani) walioshiriki kwenye mafunzo ya siku moja ya kutoa elimu
kwa Redio za jamii nchini juu ya kuandaa vipindi vyenye ujumbe sahihi
wa masuala yanayohusu watu wenye Albinism iliofanyika katika kituo cha
Redio Jamii Sengerema hivi karibuni. Katikati ni Afisa mtetezi na
ushawishi kutoka shirika linaloshughulika na watu wenye Albinism la
Under The Same Sun (UTSS), Kondo Seif na kulia ni Ofisa Miradi ya
Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu
na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.
Na modewjiblog team, Sengerema
Ofisa
mtetezi na ushawishi kutoka shirika linaloshughulika na watu wenye
Albinism la Under The Same Sun (UTSS) Kondo Seif, ameitaka jamii
kuungana kupiga vita imani potofu zinazosababisha mauaji kwa watu wenye
albinism.
Alisema jamii ikiamka na kuamua kumaliza tatizo hilo, mauaji hayo yatakoma.
Kauli
hiyo aliitoa katika semina ya siku moja ya elimu kwa Redio za jamii
nchini juu ya kuandaa vipindi vyenye ujumbe sahihi ya masuala
yanayohusu watu wenye Albinism iliofanyika katika kituo cha Redio Jamii
Sengerema mkoani Mwanza hivi karibuni.
Kondo
alisema katika jamii kumekuwa na imani potofu ambapo Albinism wamekuwa
wakiitwa majina yanayolenga kunyanyapaliwa na kusababisha kushamiri kwa
vitendo vya ukatili na mauaji dhidi yao.
Aliitaka
jamii kutambua kuwa albinism ni hali ya ukosefu wa rangi asilia mwilini
inayoathiri ngozi, macho na nywele na ni nadra hali hiyo kupatikana na
haiambukizi kama watu wengine wanavyodhani.
Aidha
ametaja jina sahihi la Kiswahili lililokubaliwa na baraza la Kiswahili
Tanzania kuitwa watu wenye albinism kuwa ni watu wenye ualbino.
Alisema
watu wenye ualbino wamekuwa wakikabiliwa na changamoto za kukosekana
kwa taarifa sahihi zinawagusa wao kama ngozi kushindwa kuhimili jua,
uoni hafifu na kupungua kwa usalama.
Kwa
mujibu wa Takwimu za shirika hilo watu wenye Albinism zaidi ya albino
70 nchini Tanzania wameuawa, zaidi ya 30 wamekatwa viungo vyao na
makaburi ya watu wenye Albinism 20 yamefukuliwa.
Ameviomba
vyombo vya habari kushiriki kikamilifu kutoa elimu sahihi kwa jamii ili
kustawisha maisha ya watu wenye Albinisms kuwa kufanya hivyo maendeleo
yao, jamii na taifa kwa ujumla yataimarika.
Awali
akizungumza na washiriki wa semina hiyo Ofisa Miradi ya Mawasiliano,
Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni
(UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph aliwataka waandishi wa habari kuzingatia
matumizi sahihi ya lugha wanapoandika habari na kuandaa vipindi
vinavyozungumzia masuala ya Albinism.
Pia
amesisitiza kuandaa vipindi vinavyobeba ujumbe sahihi wa kuelimisha
jamii juu ya masuala yanayohusu Albinism ili kubadilisha mitazamo ya
jamii ili kuwathamini, kuwalinda, kuwaheshimu na kuwashirikisha katika
maendeleo.
Sambamba
na hilo amevitaka pia kubeba jukumu kubwa la kuhamasisha wananchi
kushiriki kikamilifu zoezi la uandikishaji katika daftari la kudumu la
mpiga kura na kutoishia kujiandikisha tu bali wajitokeze kupiga kura
kuwachagua viongozi ambao ni Madiwani, Wabunge na Raisi October 2015
pamoja na kuipigia kura katiba inayopendekezwa wakati ukifika.
Ameongeza
katika matukio hayo muhimu ya kitaifa watu wenye Albinism wahamasishwe
kushiriki kikamilifu vile vile na makundi mengine kama wanawake, vijana,
watu wenye ulemavu, wazee na makundi mengine maalum.
Ofisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph akielezea
dhima ya UNESCO kuwashirikisha shirika la Under The Same Sun (UTSS)
kutoa elimu kwa Redio jamii ili kupaza sauti kwa jamii dhidi ya mauaji
ya watu wenye Albinisim pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili
walemavu wa ngozi.
Mshauri
na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akitoa mwongozo kwa washiriki
wa semina hiyo.
Afisa
mtetezi na ushawishi kutoka shirika linaloshughulika na watu wenye
Albinism la Under The Same Sun (UTSS), Kondo Seif akiendesha mafunzo
kwa mameneja wa Redio jamii nchini (hawapo pichani) kwenye semina ya
siku moja iliyofanyika wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza. Katikati ni
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.
Meneja
wa Redio jamii Mpanda FM iliyopo mkoani Katavi, Prosper Kwigize
akichangia maoni yake kwenye semina hiyo namna ya kudhibiti mauaji ya
watu wenye Albinism iliyofanyika hivi karibuni wilayani Sengerema mkoa
wa Mwanza.
Meneja
wa kituo cha Redio Jamii FADECO ya wilayani Karagwe, Adelina Lweramula
akielezea jitahada za kituo chake cha Redio kinavyoshiriki katika
kukemea mauaji ya watu wenye Albinism kwa kuendesha midahalo mbalimbali
pamoja na makala maalum kuhusiana na walemavu wa ngozi.
Baadhi
ya mameneja wa vituo vya Redio jamii nchini walioshiriki semina hiyo ya
siku moja wakifuatilia kwa umakini mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na
Bwana Kondo Seif (hayupo pichani) wa Shirika la Under The Same Sun
(UTSS).
Mkufunzi
wa semina ya siku moja kwa Mameneja wa Redio jamii nchini Kondo Seif
akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
No comments:
Post a Comment