Pages

May 9, 2015

BASI LA DAR EXPRESS LAWAKA MOTO MCHANA WA LEO

Moshi ukifuka kufuatia ajali ya basi mali ya Kampuni ya Dar ex Press lenye namba za usajili T833 DDR likiwaka moto na kuteketea kabisa hii leo majira ya saa 7:30 mchana katika kijiji cha Kwamakocho,Kata ya Mandera, Tarafa ya Miono, Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani. 

Basi hilo lilikuwa linatoka Dar es Salaam kwenda Arusha. Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika ajali hiyo. 

Akizungumza na Father Kidevu Blog, Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, SACP. Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo ni hitilafu ya umeme wa gari iliyotokea.

Aidha Kamanda Matei amesema kuwa abiria walisurika pamoja na mizigogo yao ya mikononi ila mizigo iliyokuwa katika mabuti ya basi hilo iliteketea.

Mnamo mwezi Januari mwaka huu basi lingine la kampuni ya Hajees lenye namba za usajili T 834 BAU lililokuwa likitokea handeni kwenda Dar es Salaam liliacha njia na kupinduka na kusababisha vifo vya watu wa nne katika kijiji jirani cha Mnazi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...