Pages

April 24, 2015

SERIKALI YAONYA WANAOTOROSHA MADINI

Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene akipata maelezo ya sekta ya madini

  Na Woinde Shizza,Arusha 
Serikali imewataka wachimbaji na wanunuzi wa madini ya Tanzanite nchini, kuacha tabia ya Utoroshaji wa madini hayo nje ya nchi huku,ikiagizwa kuachwa kuuzwa madini ghafi.
Katika kudhibiti biashara hiyo, serikali kwa kushirikiana na kituo cha mikutano cha Arusha(AICC) inakusudia kuanzisha kituo cha kisasa cha kimataifa cha ukataji wa madini hayo na kuuzwa nje.

Waziri wa nishati na majini George  Simbachawene alitoa wito huo , wakati akifungua  maonesho ya Kimataifa ya  nne ya madini ya Vito jijini hapa yanayoendelea  Mount Meru hoteli.

Waziri Simbachawene alisema, tabia  utoroshaji wa madini hayo inaikosesha serikali mapato na pia inawapunguzia mapato wauzaji wa madini hayo na hivyo wote kupata hasara.

Akizungumza  juu ya kituo mauzo ya madini hayo, alisema, kinatarajiwa kuwa cha kisasa, kitakachokuwa na ofisi za kodi za mapato, kiwanja kidogo cha ndege na ofisi za wauzaji na wanunuzi wa madini.
Wakizungumzia maonesho hayo, Wakurugenzi wa kampuni ya Tanzanite one, Faisal Juma na Hussein Gonga walieleza yamekuwa na manufaa makubwa na kuongeza wanunuzi wa madini.
Faisal alisema kampuni yake, imeanzisha mafunzo ya kufundisha vijana kukata madini hapa nchini ili kupunguza kuuzwa nje madini ghafi.
Naye Gonga alisema kuwa kampuni hiyo, pia itaendelea kushirikiana na serikali kuongeza ajira kwa vijana na pia kuzuia kutoroshwa nje madini hayo.


Kamishina wa madini,muhandisi Masanja amewata wamiliki wa madini,wachimbaji pamoja na wauzaji kutojiingiza katika utoroshaji wa madini kwakua unasababisha anguko la soko hilo kutokana na kupoteza bei halali ya madini hayo.

Alisema serikali itaendelea kuboresha maonesho hayo, kila mwaka na kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha biashara ya madini ya vito katika Afrika.

Maonesho hayo, yanashirikisha zaidi ya mataifa manane na wanunuzi kutoka nchi za Ulaya na Marekani mwaka  katika maonesho ya mwaka jana kiasi cha Tsh 3.4 bilioni kilipatikana 
habari picha kwa hisani ya woindeshizza blog

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...