Mbunge wa jimbo la Karatu mkoani Arusha mchungaji Israel Natse wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) ambaye pia Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini akihutubia
wananchi wake katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa mazingira
bora karatu mjini jana,amewataka wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa
wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ambayo
itawapa fursa ya kuwachagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi mkuu
unaotarajia kufanyika ockoba mwaka huu. (Habari picha na Jamiiblog).
Mbunge wa jimbo la Karatu mkoani Arusha mchungaji Israel Natse wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) ambaye pia Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini akiwa anateta jambo meza kuu.
Wananchi waliojitokeza kwa wingi wakiwa wanamsikiliza Mbunge wao akihutubia mkutano wa hadharakatika uwanja wa mazingira bora karatu mjini
Mbunge wa jimbo la Karatu mkoani
Arusha mchungaji Israel Natse akiwa anasisitiza jambo jukwaani ambapo
alisema njia bora ya kuwapiga chini chama cha mapinduzi CCM ni kwa
kuhakikisha wananchi wanajiandikisha katika daftari la kudumu huku
akidai safari hii ni jino kwa jino hadi Ikulu.
Mwenyekiti
wa vijana Wilaya ya Karatu, John Male alisema lengo lao ni kuwaelimisha
wananchi hata wasio wanachama kuhusu umuhimu wakujiandikisha katika
daftari la kudumu la wapiga kura.
Diwani
wa Kata ya Karatu mjini, Jublate Mnyenye aonya redio mbao zinazosambaza
habari kuwa anampango wa kuihama chama cha demokrasia na
maendeleo(CHADEMA)adai yeye na chama hicho ni damu damu.
Wananchi wakimshangilia Mbunge wao.
No comments:
Post a Comment