Meneja
Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu (kushoto), akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu
uboreshaji wa ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri hiyo. Kulia ni Meneja
Kodi Majengo, Stellah Mgumia.
Meneja Kodi Majengo wa Manispaa hiyo, Stellah Mgumia akitoa ufafanuzi mbalimbali wa ukusanyaji wa mapato.
Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika wa Manispaa hiyo, Francis Luambano (kushoto), akizungumza na wanahabari katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
MANISPAA
ya Ilala imewaonya wafanya biashara wanaotumia madalali kulipia huduma
zinazopatikana katika manispaa hiyo waache maana wamekuwa chanzo cha
upoteaji wa mapato katika manispaa hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano wa Manispaa
hiyo Tabu Shaibu alisema uboreshaji wa mapato unategemea sana uaminifu
wa walipa kodi kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato
vinavyotegemewa katika manispaa hiyo.“Halmashauri
ya Manispaa ya Ilala inategemea mapato yake kutoka kwa wafanya biashara
na wamiliki wa nyumba waaminifu wanaolipa kodi kwa wakati ili
kutekeleza shughuli za maendeleo”.
Shaibu
alisema manispaa inategemea vynzo vinne vya mapato ambavyo ni kodi ya
majengo, leseni za Biashara, ushuru wa mabango na kodi ya huduma za
jiji.
Kodi
nyingi imeishia mikononi mwa watu wanaojiita madalali au vishoka sababu
ya kukosa uaminifu kwa wale waliowatuma na kuingiza waliowatuma katika
hatia ya ukwepaji kodi, aliongeza Shaibu.
“Walipa
kodi wengi wamejikuta hatiani baada ya kuwatumia madalali au vishoka
wasio waaminifu kulipa kodi na kujikuta stakabadhi zao hazipo katika
kumbukumbu ya stakabadhi za manispaa za walipa kodi na kusababisha
walipe faini mara tatu ya kodi au kushtakiwa mahakamani kwa kosa la
kughushi”.Shaibu
alielezea zoezi la tathmini ya majengo ya biashara na makazi
linaliendelea katika manispaa hiyo ili kujipanga ma ukusanyaji wa kodi
wa mwaka wa fedha 2015/16 unaoanza tarehe mosi julai.
“Tunaomba
ishirikiano kutoka kwa wakazi wa wilaya ya Ilala ili tuweze kupata
makadirio ya kodi ya kodi ya majengo ambayo ni asilimia 0.15 kwa jengo
la makazi na asilimia 0.20 kwa jengo la biashara”.Shaibu
ametoa wito kwa walipa kodi kuhakikisha wanalipa kodi kwenye mamlaka
husika na kama walishatumia madalali au vishoka wakahakiki nyaraka zao
manispaa ili wasije kuingia matatizoni.”
(Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/
No comments:
Post a Comment