Hizi ndivyo lori hilo lilivyoharibika
WATU
watatu waliokuwa wamepakizana mishikaki wamekufa kwa kuteketea kwa moto
mjini Iringa usiku huu baada ya usafiri aina ya pikipiki (Boda
boda)waliyokuwa wakisafiri kutoka mjini Iringa kuelekea Nduli nje kidogo
na mji wa Iringa kugongana na lori aina ya Fuso na kupelekea pikipiki
hiyo kuwaka moto.
Ajali
hiyo imetokea wakati boda boda hiyo ikiwa
katika mwendo mkali kugongana na lori hilo ambalo pia lilikuwa katika
mwendo na kusababisha vifo hivyo .
Mashuhuda
wamesema kuwa kijana mmoja ambae inasadikika ndie dereva wa boda boda
hiyo ametambuliwa kwa jina moja la Julius huku wengine wawili bado
kutambuliwa .
Miili ya marehemu hayo imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa utambuzi zaidi
No comments:
Post a Comment