Pages

February 4, 2015

MBUNGE JOSHUA NASSAR AWAONGOZA WANANCHI KATIKA MAKABIDHIANO YA HEKARI 92 ZA SHAMBA LA MADIIRA ARUMERU


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru,Dastan Malya akiwa na watendaji wengine wa serikali katika ofisi ya mtendaji wa kata ya Siela Sing’isi wakati mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar alipofika kwa ajili ya kwenda kutembelea Shamba la Madiira.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari akitia saini katika kitabu cha wageni katika ofisi ya kata ya Seela Sing'isi alipotembelea katika kijiji hicho cha Sing'isi.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar akiongozana na Diwani wa kata ya Mbunguni Paul Laizer maarufu kama Askofu (shoto) wakati alipowaongoza wakazi wa vijiji vya Sing'isi na Malala kwenda kuangalia shamba la Madiira ambalo hekari 92 zimetolewa kwa vijiji hivyo.
Wananchi wa vijiji vya Sing'isi na Malala wakitizama sehemu ya eneo la Shamba la Madiira lililotolewa kwa wananchi wa vijiji hivyo.
Mpima wa Halmashauri ya wilaya ya Meru ,Seveline Luambano akiwaonesha wananchi wa vijiji vya Sing'isi na Malala,mipaka pamoja na michoro ya ramani ya eneo la hekari 92 zilizotolewa kwa vijiji hivyo .zoezi hilo limeshuhudiwa na Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar.
Wananchi wakiwa katika Shamba la Madiira kutizama mipaka ya eneo ambalo limetolewa kwao.
Sehemu ya Shamba la Madiira.
Mbunge Nassari akiwaongoza wananchi wa vijiji vya Sing'isi na Madiira wakitembelea shamaba la Madiira kutizama mipaka ya eneo la Hekari 92 lililotolewa kwao.
Mbunge Nassari akimsikiliza Mwenyekiti wa kijiji cha Sing'isi  Elishiria Kimoto akitoa maelezo ya kusitishwa kwa zoezi la kuoneshwa eneo hilo hadi pale Maofisa Ardhi wa Halamashauri hiyo watakapo weka mionundo mbuni ya barabara katika eneo hilo.
Mbunge Nasari akizungumza na wananchi wa vijiji hivyo mara baada ya kutembelea maeneo kadhaa ya eneo la Shamba la Madiira ambao aliwataka kusitisha kilimo ili kuruhusu maofisa Ardhi kupitishwa greda kwa ajili ya kuchonga barabara pamoja na mitaa katika eneo hilo.
Wananchi wakiwa katika kikao cha pamoja.
Na Dixon Busagaga wa Globu

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...