Baadhi ya Wahitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar wakiingia katika Viwanja vya Mahafali chuoni hapo.
Mgeni
Rasmi katika Mahafali ya Sita ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar
Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Saada
Mkuya akitoa hotuba kwa wahitimu hawapo pichani ambapo mewataka
wajiajiri wenyewe badala ya kutegemea Serikali.
Baadhi
ya Wahitimu wa Fani ya Upishi wakiwa wanamsikiliza Mgeni Rasmi Waziri
wa Fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Saada Mkuya
hayupo pichani wakati wa sherehe ya Mahafali ya Sita ya Chuoni hapo.
Baadhi
ya Wahitimu wa Fani ya Ukarimu na Uongozi wa Hoteli wakivaa kofia
kuashiria kukabidhiwa Stashahada zao katika Mahafali ya sita ya Chuo cha
Maendeleo ya Utalii Zanzibar.
Mwanafunzi
Bora Chuoni hapo wa Fani ya Mapokezi ya Wageni “Front Office”Said
Shaame Khamis akipokea Zawadi kutoka kwa Mgeni Rasmi Waziri wa fedha wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Saada Mkuya katika Mahafali
hayo
Yaliyofanyika Maruhubi mjini Zanzibar.
Mgeni
Rasmi Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Saada Mkuya katikati mwenye miwani akiwa katika Picha ya pamoja na
viongozi wachuo na Wahitimu wa mahafali ya sita ya Chuo cha Maendeleo ya
Utalii Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
Na Faki Mjaka- Maelezo Zanzibar 22/02/2015
Waziri
wa Fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Saada Mkuya
amewataka Wahitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar kutoitegemea
Serikali katika kupata ajira badala yake wajikite katika kujiajiri
wenyewe.
Amesema
nafasi za Ajira Serikalini ni chache hivyo Wahitimu hao wanapaswa
kujishughulisha ili wajiajiri wenyewe au kupitia Taasisi Binafsi.
Waziri
Mkuya ameyasema hayo alipokuwa akitoa hutuba yake kwa Wahitimu wa
Mahafali ya Sita ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii yaliyofanyika leo kati
viwanja vya Chuo hicho Maruhubi Mjini Zanzibar.
Amesema
dhana ya kuitegemea Serikali katika ajira kwa sasa haina nafasi
kutokana na uchache wa Ajira na kwamba anaamini Elimu waliyoipata
Wahitimu inaweza kuwasaidia katika kujiajiri.
Ametoa
Rai kwa Wahitimu hao kujiunga na Kampuni za Ulinzi ambazo zinatarajiwa
kuanzishwa Zanzibar kutokana na kuripotiwa kwa matukio mbalimbali ya
kihalifu nchini.
Aidha
Waziri Mkuya amewashauri Wahitimu hao kutotosheka na kiwango cha Elimu
walichofikia badala yake wajiendeleze mbele ili kupata ufanisi katika
kazi zao.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Chuo hicho Bi Zulekha Khamis Omar amesema Chuo
hicho kinazidi kupiga hatua kimaendeleo nakwamba Wanatarajia kuanzisha
Masomo ya Shahada ya Kwanza mwaka 2017-18.
Amesema
mipango ipo mbioni kukamilika kuhusu kuanzishwa kwa Masomo ya Shahada
ambapo Chuo hicho kitakuwa Chini ya Chuo Kikuu cha Zanzibar SUZA.
Hata
hivyo Bi Zulekha alizitaja Changamoto zinazokabili Chuo hicho kuwa ni
pamoja na Uhaba wa Vifaa katika Jiko, na Mmommonyoko wa Ardhi unaotishia
Mazingira ya Chuo hicho.
Chuo
hicho kilichoanzishwa mwaka 1992 ili kuongeza ukuaji na Maendeleo ya
Utalii Zanzibar kimefanya Mahafali yake ya sita ambapo Jumla ya Wahitimu
511 wa Ngazi za Stashahada na Cheti katika Fani mbalimbali wamehitimu.
No comments:
Post a Comment