Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (Tamisemi) Hawa Ghasia
Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na serikali za
Mitaa (Tamisemi) Hawa Ghasia amewasimamisha kazi wakurugenzi wa
halmashauri mbalimbali kutokana na kuchelewa kuandaa na kupeleka
vifaa vya kupigia kura pamoja na uzembe katika kutekeleza majukumu yao
katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika nchi nzima Jumapili
iliyopita.
Akizingumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, waziri Ghasia amesema
uamuzi huo umefanyika baada ya Rais kwa mujibu wa sheria kuridhia adhabu
hizo zitolewe.
Alisema wakurugenzi waliosimamishwa kazi ni
watano ili kupisha uchunguzi zaidi wa kiwango cha ushiriki wao katika
kasoro zilizojitokeza kwenye halmashauri zao.
Wakurugenzi
hao waliosimamishwa kazi na halmashauri zao kwenye mabano ni Fotunatus
Fwema(Mbulu), Issabela Chilumba(Ulanga), Pendo Malabeja(Kwimba), Wiliam
Shimwela(Sumbawanga Manispaa) na Felix.T.Mabula(Hanang).
Kwa
mujibu wa Ghasia, wakurugenzi ambao uteuzi wao umetenguliwa ni sita na
watapangiwa kazi za kufanya kutokana na taaluma zao huku Wakurugenzi
watatu wakipewa onyo kali na watakuwa chini ya uangalizi kama
wanaudhaifu wachukuliwe hatua Zaidi.
Aliwataja wakurugenzi
watendaji waliotenguliwa nyadhifa zao ni Benjamin Mjoya aliyekuwa
Kaimu Mkurugenzi (Mkuranga), Abdalla Ngodu(Kaliua),Masalu Mayaya
(Kasulu), Goody Pamba (Serengeti), Julius Madiga (Sengerema) na Simon
Mayeye (Bunda).
Aliwataja wakurugenzi waliopewa onyo kali
ni pamoja na Mohamed Maje (Rombo),Hamis Yuna (Busega) na Jovin
Jungu(Muheza) na watakuwa chini ya uangalizi kubaini kama wana udhaifu
mwingine wachukuliwe hatua Zaidi.
Waziri Ghasia alionya kuwa
ofisi yake haitasita kuchukua hatua stahiki kwa wote watakaokiuka
maadili ya kazi au watakaopungukiwa uwezo wa kutekeleza majukumu
waliokabidhiwa.MWANANCHI
No comments:
Post a Comment