Wafanyakazi wa Lake Duluti
Serena Hotel wakitoa zawadi mbalimbali kwa watoto hao. |
Meneja wa Lake Duluti Serena Hotel,Gerald Macharia(kulia)akitoa zawadi ya jiko la Gas kwa mlezi wa Nyumba hiyo Damari Mbisse. |
Mwandishi
Wetu,Arumeru
Watoto
wanaolelewa katika nyumba ya watoto katika hospitali ya Nkoaranga wamepewa
misaada mbalimbali iliyotolewa na wafanyakazi wa Lake Duluti Serena
Hotel,mkoa wa Arusha katika kusherekea siku kuu za Krismas na mwaka mpya ikiwa
ni njia ya kuyakumbuka makundi maalumu katika jamii.
Meneja
wa hoteli hiyo, Gerald Macharia amesema wameguswa na hali ya maisha ya watoto
hao ambao wazazi wao walifariki dunia wakati wa kujifungua na wengine
walitelekezwa baada ya kuzaliwa.
Amesema
kwa miaka iliyopita walikua na utaratibu wa kutumia gharama kubwa kupamba hoteli
wakati wa Siku kuu za mwisho wa mwaka ila kwanzia mwaka jana waliamua kuwa
watakua wanatoa misaada kwa jamii zenye mahitaji maalumu.
“Wafanyakazi
na marafiki zetu tulitoa misaada katika Shule ya Msingi yenye mahitaji maalumu
ya Patandi iliyopo wilaya ya Arumeru, tuliguswa sana na kuona tuna wajibu wa
kushirikiana na wadau wengine kuifikia jamii kwa misaada mbalimbali”amesema
Macharia
Nkoaranga
Hospital Children’s Home ina jumla ya watoto zaidi ya 70 na ilianzishwa mwaka
1965 ikiwa na watoto wenye umri wa miezi 3 hadi miaka 8 huku wakipata
elimu katika viwango tofauti.
No comments:
Post a Comment