Naisola Mbeeya(kushoto) ambaye ni mwanachama wa kikundi cha Naitobo wilayani Ngorongoro mkoa wa Arusha akionesha urembo wa asili wa jamii hiyo na Asali. |
Wanakikundi cha Ujasiriamali kutoka wilaya ya Ngorongoro,mkoa wa Arusha wakionesha asali iliyowekwa kwenye vifungashio bora. |
Mjasiriamali aliyepata mafunzo kutoka taasisi ya Farm Africa,Dareda wilaya ya Babati mkoa wa Manyara. |
Mwandishi Wetu,Arusha
Wafugaji
wa Nyuki wilayani Ngorongoro wameiomba serikali iwasaidie kupata
masoko ya uhakika ya kuuza zao la Nyuki na Asali,kwa kuwa changamoto
hiyo imekuwa ikiwakabili kwa muda mrefu, hatua ambayoimechangia
kwa wafugaji hao kutoona umuhimu wa kuzalisha zao hilo kwa wingi.
Aidha
wamesema vitendea kazi wanavyotumia wakati wa kurina asali ,kuhifadhi
na kuzalisha zao la Nta ni duni ,suala ambalo wameiomba
serikali kuangalia uwezekano wa kuwapatia vifaa hivyo ili kuongeza
tija katika uzalishaji na utunzaji wa mazingira.
Wakizungumza
na katika kongamano la kwanza la ufugaji
nyuki barani Afrika linalofanyika jijini hapa,wamesema ipo haja
kwa serikali ya Tanzania kuviwezesha vikundi mbalimbali vinavyojishughulisha
na ufugaji nyuki .
Mkazi
wa kitongoji cha Ngwaile,wilayani Ngorongoro,Abraham Molelulu amesema
kuwa wamekuwa wakifuga nyuki kwa muda mrefu,baada ya kuwezeshwa
mizinga 60 kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA).
Amesema
asali inayopatikana wamekuwa wakiitumia kubadilishana na mazao wao
kwa wao kwa matumizi ya dawa na chakula kwa wakati wa kiangazi na wamekuwa
wakibadilishana kwa mifugo kama ng’ombe na mbuzi na pia huitumia
kwa wakati wa sherehe.
Ameongeza
kuwa changamoto kubwa ni kupatikana kwa masoko,vifaa vya kuchujia na
kutengeneza zao la Nta,pamoja na elimu juu ya manufaa ya Nta, aliongeza
kuwa pamoja na kushiriki katika maonyesho mbalimbali lakini bado
wanakabiliwa na ukosefu wa vifaa vya kutengeneza mshumaa inayotokana
na Nta.
Kwa
upande wa afisa utalii wa NCAA,Edward Ngobei,amesema mamlaka
hiyo imekuwa ikiendeleza utalii wa aina mbalimbali katika hifadhi
hiyo,pia kuendeleza jamii inayoishi ndani ya mamlaka hiyo ikiwemo
Wamasai,Wadzabe na Wabarbaig
Amesema
mamlaka hiyo imekuwa ikisimamia vikundi zaidi ya 14 vya makabila
hayo kwa kuviwezesha kufanikisha shughuli za ufugaji wa nyuki kwa
kuvipatia mizinga ya Nyuki,kutoa elimu ya ufugaji nyuki na kulinda mazingira.
Aliongeza
kuwa mamlaka hiyo imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya kuendeleza
ufugaji nyuki na mkakati mkubwa ni kuboresha usindikaji wa Nyuki
ili uwe kwenye kiwango cha kimataifa.
No comments:
Post a Comment