Pages

November 10, 2014

TANZANIA 2O14 KUJIVUA TAJI MAPYA YAIBUKA


Miss Tanzania 2014 aliyevuliwa taji, Sitti Abbas Mtemvu akipanda jukwaani kupata maombi ya Nabii Yaspi Bendera.
Stori: Chande Abdallah, Deogratius Mongela na Musa Mateja.
TENA! Saa chache tu baada ya Miss Tanzania 2014 aliyezua tafrani la kuchakachua umri kwa kujipunguzia miaka 2 ya kuzaliwa, Sitti Abbas Mtemvu kujisalimisha kwa kujivua taji mwenyewe, mapya yameibuka na Ijumaa Wikienda lina mzigo mkononi!

Mapya hayo yameibukia ndani ya Kanisa la Revelation Church lililopo Buza–Kipera jijini Dar kwa Nabii Yaspi Bendera ambaye amezungumzia ishu ya Sitti kujivua  taji mwenyewe.“Alikuja kwangu nikamwombea, akapata taji. Hata alipopata alikuja kushukuru, nilimwambia aendelee kudumu kwangu hadi atakapokwenda kwenye taji la dunia (Miss World) lakini hakufanya hivyo, akawa haji tena.“Hivi, nitoe mfano mmoja. Kama mtu akienda kwa mganga kuomba apewe dawa ili apate ujauzito, akishapata akaenda kwa mganga mwingine kuomba amfanyie dawa ili ujauzito huo usitoke. Je, siku ukitoka nani analaumiwa, mganga wa kwanza au wa pili?”
Aliyekuwa Miss Tanzania 2014 akipokea maombi ya nguvu kutoka kwa Nabii Yaspi Bendera

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...