Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Nishati na Madini,Mhandisi Ngosi
Mwihava(katikati)akikata utepe kufungua Maonesho ya Tatu ya Madini ya Vito ya
kimataifa mkoani Arusha leo.
|
Kamishna wa Madini nchini,Mhandisi Paul Massanja(kushoto)akimpongeza mmoja wa wafanyabiashara ya madini ya Vito jijini Arusha. |
Viongozi mbalimbali wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara kutoka nchini DRC. |
Mwandishi
wetu,Arusha
Serikali
imekua ikipoteza mapato mengi kutokana na utoroshwaji wa madini aina ya
Tanzanite yanayopatikana nchini Tanzania pekee.
Kamishna
wa Madini nchini,Eng Paul Massanja amesema leo wakati wa maonesho ya madini ya
Vito yanayofanyika jijini hapa ambayo yanahudhuriwa na washiriki kutoka mataifa
mbalimbali.
Amesema
kwa takwimu za mwaka 2013,Tanzania ilipata dola za marekani 38 milioni wakati
nchi ya Kenya ilijipatia kiasi cha dola 100 milioni na India ilijikusanyia
kitita cha dola 300 milioni.
"Wote
mnafahamu haya madini yanapatikana Tanzania pekee huu ni ushahidi kuwa kumekuwa
na utoroshwaji wa madini haya kwa kiwango kikubwa jambo linalotunyima mapato ya
kutosha"anasema Eng Massanja
Hata
hivyo amesema wataendelea kudhibiti mianya ya utoroshaji wa madini nje ya nchi
ambayo hayajaripiwa kodi sitahili huku kukiwa na mipango ya kujenga jengo kubwa
ambalo litatumika kufanyia biashara ya madini.
No comments:
Post a Comment