Pages

November 10, 2014

RAIS WA BUNGE LA SADC NA SPIKA WA BUNGE LA TANZANIA MHE. ANNE MAKINDA ASHIRIKI MISA MAALUM YA KUMWOMBEA ALIYEKUWA RAIS WA ZAMBIA MAREHEMU MICHAEL SATA KATIKA VIWANJA VYA BUNGE LA ZAMBIA MJINI LUSAKA LEO

Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwasili katika viwanja vya Bunge la Zambia tayari kushiriki Misa Maalum ya Kumwombea aliyekuwa Rais wa Zambia Mhe. Michael Chilufya Sata kabla ya maziko yake kufanyika hapo kesho.
Aliyekuwa Rais wa Serikali ya Zambia Mhe. Lupia Banda akimpokea Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda alipowasili katika viwanja vya Bunge la Zambia tayari kushiriki Misa Maalum ya Kumwombea aliyekuwa Rais wa Zambia Mhe. Michael Chilufya Sata kabla ya maziko yake kufanyika hapo kesho.
Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akisalimiana na Rais wa Kwanza wa Zambia Dkt. Kenneth Kaunda mara baada ya Kuwasili katika Viwanja vya Bunge kushiriki Misa hiyo.
Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akishiriki Misa Maalum ya kumwombea aliyekuwa Rais wa Zambia Mhe. Michael Sata katika viwanja vya Bunge la Zambia leo. Mwili wa Marehemu Sata unatarajia kuzikwa kesho mjini Lusaka.
Mwili wa aliyekuwa Rais wa Zambia marehemu Michael Sata ukiwasili katika viwanja vya Bunge la Zambia leo tayari kwa misa Maalum iliyoandaliwa kabla ya mazishi kufanyika hapo kesho.
Mjane wa aliyekuwa Rais wa Zambia Dkt. Christine Kaseba Sata akiliwazwa na mke wa kaimu Rais wa nchi hiyo Bi. Charlote Scot wakati wa Misa hiyo.
Kaimu Rais wa Zambia Mhe. Guy Scot (kulia) akishiriki Misa hiyo.
Kaunda akitafakari kwa huzuni kifo cha Sata.
Kutoka kushoto ni Dkt. Kenneth Kaunda, Lupia Banda na Anne Makinda wakiwa na huzuni tele.
MC akiongoza misa hiyo.
Makinda akihojiwa na Waandishi mara baada ya kumalizika kwa misa hiyo.
Rais wa Bunge la SADC na ambaye ni Spika wa Bunge la Tanzania akiondoka katika viwanja vya Bunge la Zambia na Mwenyeji wake Dkt. Patrick Matibini, Spika wa Bunge la Zambia. Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...