Mrembo
aliyetawazwa umalkia wa Tanzania 2014, 'Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas
Mtevu (pichani kushoto) leo ametangaza rasmi kujivua taji hilo. Pamoja
nae ni Mkurugenzi wa Lino International Agency Hashim Lundenga, ambao
ndio waandaaji wa Miss Tanzania akizungumza japo katika moja ya mikutano
na waandishi ambayo ilihusiana na taji hilo la Miss Tanzania 2014
kushikiliwa na Sitti ilhali anashutumiwa kudanganya umri.
Pasi nakuwepo mrembo huyo Lundenga, alisoma barua iliyoandikwa na
mrembo huyo na kubainisha kuwa, Sitti Mtemvu ameamua kulivua
taji hilo kwa hiari yake mwenye bila shinikizo ili kuepukana na maneno ya
kumchafua dhidi yake na kuilinda heshima yake, ya familia ya Mtemvu na Kamati ya Miss Tanzania.
"Sasa
kwa hiari yangu mwenyewe tena bila ya kushawishiwa na mtu, na kwa
kulinda heshima yangu, pamoja na familia yangu natamka rasmi kuvua taji
la Miss Tanzania 2014," ilisema sehemu ya barua hiyo.
Sitti katika barua yake hiyo kuwa tangu
kushinda taji hilo kumezuka
shutuma mbalimbali dhidi yake, wamemuwekea maneno mengi sana mdomoni
kwamba ameyasema wakati siyo, shutuma hizo zimekuwa zikiandikwa katika
vyombo vya
habari, blogs na mitandao ya kijamii kiasi ambacho ameona kinaweza hata
kuhatarisha maisha yake.
Uamuzi wa
kujivua taji hilo uliandikwa katika barua iliyotumwa kwenye kamati ya
mashindano ya Miss Tanzania tangu Jumatano ya wiki hii, ambapo Lundenga alisema
kuwa wamekubaliana na ombi la mrembo huyo.
Kamati ya Miss Tanzania imemvika rasmi
taji hilio Mrembo aliyekuwa am,eshika nafasi ya pili, Lilian Kamazima na
sasa ndiye Miss Tanzania 2014.
No comments:
Post a Comment