Mwandishi Wetu,Arusha
Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika(AfCHR) yenye makao yake jijini Arusha,Tanzania imesema inakabiliwa na changamoto ya kutokufahamika kwa wananchi wengi Afrika huku kikwazo kikiwa ni uchache wa nchi 28 pekee zilizoridhia na kusaini Itifaki kati ya nchi 52.
Naibu Msajili wa Mahakama hiyo ambaye ni raia wa Burkina Faso,Nouhou Diallo amesema hayo leo wakati akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha African Nazarene University(ANU)cha nchini Kenya waliofika kujifunza namna taasisi hiyo inavyotimiza wajibu wake.
Amesema kati ya nchi hizo 28 ni 7 pekee zilizotoa tamko la kuridhia Watu binafsi na Asasi za kiraia kufungua kesi dhidi ya nchi zao katika mambo yanayohusiana na ukikwaji wa haki za binadamu.
"Hii ni changamoto kubwa kama unavyojua hali ya ukiukwaji wa haki za binadamu ilivyo katika Bara la Afrika,tunahitaji kuona nchi nyingi zikitoa tamko kuruhusu raia wake na Asasi zisizo zikipata nafasi ya kufanya hivo,"alisema Diallo
Diallo amezitaka Asasi zisikuwa za kiserikali na vijana kuchochea mabadiliko chanya yatakayoleta mabadiliko halisi katika nchi za kiafrika kwa kuweka umuhimu wa kuheshimu haki za binadamu.
Kiongozi wa msafara huo ambaye ni Mhadiri Mwandamizi,Wakili James Mamboleo ameiomba mahakama hiyo kutoa elimu zaidi ya uelewa kwa wananchi hasa wanafunzi wa elimu ya juu ili ieleweke vema kwa wananchi.
Mmoja wa wanafunzi akifurahia kitabu kwenye Maktaba ya Mahakama hiyo leo |
Wanafunzi wanaosoma Sheria katika Chuo cha African Nazarene University(ANU) , Nairobi nchini Kenya wakiangalia baadhi ya Kesi zilizowahi kufunguliwa katika Mahakama hiyo. |
No comments:
Post a Comment