Baada
ya Mwezi Oktoba kuisha ambapo kubwa lilikua ni kukuza uelewa juu ya
matumizi salama ya mitandao, Taarifa ya kumalizika kwa mwezi huo inaweza
kusomeka"HAPA" Mambo
mengi tuliyo yajadili yameonekana kuangaziwa tena kwenye kongamano la
maswala ya TEHAMA Jijini Cairo Nchini Misri. Muundo wa kongamano hili
ulihusisha meza kuu inayo fungua mijadala na wasikilizaji kuchangia na
kuuliza mwaswali pamoja na kupata njia ya kufikia malengo kupitia mada
tofauti tofauti.
Naibu
Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba, Katika
Meza kuu ya Mjadala alio husisshwa alipata kuzungumzia jinsi teknolojia
ya habari na mawasiliano inavyo patiwa kipaumbele cha mwishoni na idara
za fedha katika mataifa mbali mbali ingawa ni sekta ambayo ina nafasi
kubwa sana katika kuleta mabadiliko na kukuza kwa haraka uchumi wan chi
yeyote kama itatumika vizuri.
Aidha,
Kwenye Meza kuu ambayo Nilikua nimehusika tulipata kuangazia maswala
mbali mbali na huku nikizungumzia kwa kina jinsi usalama mitandao
utakapo achwa kupewa kipaumbele unavyo weza kurudisha nyuma jitihada za
dhati za kutumika vizuri kwa teknolojia ya Habari ili kukuza uchumi wan
chi mbali mbali.
Pia
nilipata kuzungumzia umuhimu mkubwa wa kuhakikisha mataifa ya Afrika
yanaongeza jitihada ili kuhakiki Mafunzo yahusuyo usalama mitandao
yanakuzwa kwa kasi ili kuhakiika wataalam wa kutosha wanapatikana na
kusababisha watumiao vibaya teknolojia ya habari na mawasiliano wanaweza
kuangazwa kiurahisi na kudhibitiwa kwa manufaa ya kukuza uchumi wan chi
yoyote duniani.
Katika
Mkutano Huu ambao Pia ulihudhuriwa na Mkuu wa Intel bwana John E.
Davies, Kama anavyo onekana kwenye picha akiwa na Mkuu wa Intel katika
Nchi ya Misri, Sikusita kukutana nao na kujadili maswala mbali mbali
yahusuyo usalama mitandao huku nikitaka kujua jinsi gani Intel
inajipanga kuhakiki uinzi mtandao unakua na nafasi nzuri.
Katika
Kunipatia Majiibu, Nilifarijika kujua ya kua Intel imejipanga kuweka
ulinzi mtandao katika vifaa vyake ambavyo kwa kushirikiana na program za
Anti-virus kwa pamoja zitaimarisha ulinzi wa kina katika Komputa.
Alinihakikishia hatua yao hiyo haita punguza soko la matumizi ya
Anti-virus bali kwa pamoja patapatiwa namna ya kuongeza nguvu ili
kukabiliana na wimbi la virusi vinavyo tumwa kwenye Komputa za watumiaji
ili kuleta athar.
Aidha,
Kwa Upande wa Waziri mwenye dhamana ya Sayansi na Teknolojia Nchini
Misri, Enginia Atef Helmy mbali na kuonyewha kufurahi sana kuona mimi
nilifanikisha kuhudhuria mkutano huo alinieleza anajitihada za dhati
kuhakikisha panapatikana daraja madhubuti la kuunganisha Afrika kuanzia
kusini hadi kazkazini.
Aliifafanua
na kusema kwa kushirikiana Nchi za Afrika katika maswala ya Tehama na
pia kuimarisha nguvu ya pamoja anaimani kabisa teknolojia ya Habari na
mawasiliano ina nafasi kubwa sana ya kuleta mabadiliko katika dunia ya
kesho. Pia alinieleza kwa kina ya kua vijana ndio hasa nguvu kazi inayo
itajika na dunia ya leo ili kuhakiki mambo yanasogea vizuri.
Mbali
na mijadala mbali mbali, Pia palikua na matukio yakutia saini
makubaliano ya kukuza ushirikiano nanchi za bara Asia pamoja na mataifa
mengine. Palipatikana Ziara maalum ya kutembelea idara maalum inayo
husika na maswala ya ulinzi wa mitandao wan hi ya Misri. Pale tulipata
kujionea shughuli mbali mbali zinazocfanyika kuhakiki Nchi ya Misri
inabaki salama mitandaoni.
Huko
mbali na kujionea mengi na matumizi makubwa ya teknolojia yanavyo
tumika kuhakiki Nchi inabaki salama kiimtandao. Tulipata kuonyeshwa
changamoto mbali mbali walizo kumbana nazo kama taifa na ukanda mzima wa
Nchi za mashariki ya kati.
Aidha,
Ufafanuzi mzuri wa namna changamoto zimetumika vizuri kuwa Fursa na
kuhakiki mambo yanasogea tulipata kujizwa. Na pia tulipata kuonyeshwa
jia mbali mbali zinazo tumika nan chi hiyo ili kuhakiki wataalam wa
maswala ya usalama mtandao wana zalishwa ipasavyo ili kuweza kukabiliana
na changgamoto za uhalifu mtandao zinazo endelea kukua kwa kasi. Mengi
yalikuua yanafanana na nilicho kizungumza na kituo cha "MLIMANI TV" ili kutolea ufafanuzi baadhi yam ambo.
No comments:
Post a Comment