Pages

November 18, 2014

KINANA ATINGA JIMBO LA MCHINGA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Mchinga Ndugu Said Mtanda wakati wa mapokezi yake yaliyofanyika Kitomanga  Mkwajuni jimboni hapo wilaya ya Lindi vijijini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi wa jimbo la Mchinga waliojitokeza kumpokea.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza wimbo maalum wa mapokezi kutoka kikundi cha uhamasishaji cha CCM Mchinga mara baada ya kuwasili Kitomanga Mkwajuni jimbo la Mchinga.
 Katibu Mkuu wa CCM akishiriki ujenzi wa ghala la kijiji ambalo litatumika kuhifadhia chakula kwa wakazi wa Kitomanga Mkwajuni
 Wananchi wa kijiji cha Namkongo wakimpokea Katibu mkuu wa CCM kwa namna yake mara baada ya kuwasili kijijini hapo ambapo alizindua mradi wa maji na kukabidhi saruji kwa ajili ya ujenzi wa soko.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa mbunge wa Jimbo la Mchinga  Ndugu Said Mtanda  namna wananchi wa kijiji cha Namkongo walivyopata tabu ya kutafuta maji

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...