JANUARY MAKAMBA USO KWA USO NA ABSALOM KIBANDA
JANUARI MAKAMBA.
Gazeti la Mtanzania leo Novemba 14 limeandikwa kichwa cha habari kinachosomeka hivi; “.. Utafiti
watibua wagombea urais 2015.. January aupinga, Zitto amwambia aache
siasa.. Keissy ashangaa Wasira kutosomeka katika ripoti..”
Kupitia mtandao wa Twitter, hiki ndicho kilichoandikwa na mhariri
Absalom Kibanda na Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia
January Makamba:
J. Makamba : “ Unaelezeaje suala la gazeti lako kunukuu kinyume kabisa na mtu alivyosema? Umeambiwa. ”
A. Kibanda : “ Nimeambiwa kaka. Badala ya kuandika JM kahoji wao wakaona umepinga utafiti.”
J. Makamba : “ Si kweli. Na nimesema specifically sipingi. Heshima ndogo niliyobakiwa nayo na Mtanzania imeisha.”
A. Kibanda : “ You judge the paper kwa kosa ambalo msingi wake ni kauli yako?! Worldwide media zinafanya makosa hayo ya tafsiri”
J. Makamba : “
makosa yanatokea, ni kawaida na yanasameheka. Kupindisha makusudi kwa
malengo mahsusi ni dhambi kwa wasomaji, tasnia na mhusika”
A. Kibanda : “ Kaka unless silijui hilo. Siwezi kuruhusu gazeti naloongoza likuhujumu wewe au mwingine yeyote. Hata awe Membe anayenichukia”
No comments:
Post a Comment