Pages

October 7, 2014

UMOJA NI NGUVU: SIMBA DUME AKILA KICHAPO KUTOKA KWA NYATI

 Simba dume amejikuta katik ahali tata baada ya kutolewa mkuku na Nyati katika Hifadhi ya Kruger, nchini Afrika Kusini, walipomfumania akiwa katika mawindo yake. Gazeti la Daily Mail la Uingereza limeripoti.
 Hakika waswahili husema mbio za sakafuni huishia ukutani na za mwizi ni 40 siku yako ikifika hata uwe mtemi vipi watakukamata tu. Simba akitimua mbio huku akifuatwa kwa kasi na Nyati.
 Nyati walimfikia na kumchota mtama wa aina yake na kukaa chini.
 Simba alinza kula za uso kama alivyonaswa na camera ya Lyle Gregg.
 Walipiga kila kona ya mwili wa simba na kujeruhi vibaya sehemu za kichwa.
Simba alipoteza kabisa ubabe wake maana mateke ya kichwa yalimuandama na pembe mithili ya wabongo wampigavyo kibaka.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...