Pages

October 12, 2014

TAARIFA YA KAMATI YA UTENDAJI YA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA ILIYOKUTANA OKTOBA 11, 2014- DAR ES SALAAM

Rais wa TFF, Jamal Malinzi
Kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kimefanyika leo kujadili matukio ya hivi karibuni, hasa mwenendo wa wadau wa Bodi ya Ligi. Shirikisho linatoa tamko kwa umma kama ifuatavyo:
  1. Kamati ya Utendaaji imesikitishwa na taarifa za upotoshaji kuhusu kanuni mpya za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), hivyo inaomba radhi kwa wadau ambao wameguswa na kusumbuliwa na matukio hayo.
2.Kufuatia matukio hayo, Sekretarieti ya TFF kwa niaba ya Kamati ya Utendaji, imefungua mashtaka kwenye Kamati ya Nidhamu dhidi ya Dk. Damas Ndumbaro ambaye ni mjumbe wa Bodi ya Ligi na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba. Pia wadau wote waliohusika na upotoshaji huo wakiwemo wafanyakazi wa TFF na Bodi ya Ligi watashughulikiwa kulingana na nafasi zao.

3.Kutokana na madai ya klabu kuhusu vipengele kadhaa vya Kanuni za Ligi Kuu 2014/15, Kamati ya Utendaji imepanga kukutana na viongozi wa klabu za Ligi Kuu siku ya Jumamosi, Oktoba 18 mwaka huu ili kuwasikiliza na kushauriana kuhusu changamoto za kikanuni na uendeshaji wa mashindano kwa ujumla.
4.Kamati ya Utendaji itaendelea kuboresha Kanuni za Uendeshaji Bodi ya Ligi (Governing Regulations) ili kuweka uwiano wa utendaji na kuepusha tofauti kati ya Bodi ya Ligi, vilabu na TFF. Aidha Kamati ya Utendaji itafanya kila linalowezekana kuboresha ligi kwa kuijengea uwezo Bodi ya Ligi kwa lengo la kuwa na ligi zinazoendeshwa kisasa (Professional Leagues).

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...