Supastaa
wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mpenzi wake,
Wema Isaac Sepetu ‘Onyinye’. Ubavu wa Diamond, Wema Isaac Sepetu
‘Onyinye’ ndiye aliyekuwa gumzo katika sherehe hiyo baada ya watu wengi
kuwa na shauku ya kuona kama atafika au la.
NI Gumzo!
Hiyo ndiyo kauli pekee inayoweza kuakisi pati ya kuzaliwa ya supastaa
wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye ametimiza umri wa
miaka 25, iliyofanyika usiku wa kuamikia jana kwenye Ukumbi wa Golden
Jubilee Tower (PSPF), Posta jijini Dar, Risasi Jumamosi lilikuwepo ndani
ya nyumba.
Wengi
walitaka kujua kama atafika, ataingia kwa staili gani kutokana na
minong’ono iliyokuwa ikiendelea kuwa huenda Wema asitokee kwenye sherehe
hiyo kutokana na madai kuwa Diamond alikasirika baada ya kukuta mpenzi
wake huyo amezawadiwa ndinga aina ya BMW 454i na Martin Kadinda hivyo
kuhoji uhalali wake.
Diamond
Platnumz, ubavu wake, Wema Sepetu na Bi mkubwa wake wakipiga picha ya
pamoja. Katika hali isiyotegemewa, Diamond na Wema waliingia pamoja huku
wakiwa wameshikana mikono.
Wema alivaa gauni lenye mpasuo wa aina yake, kila mmoja alimfuatilia hatua kwa hatua kutaka kujua atasababisha tukio gani.
Watu kibao waliohudhuria ukumbini hapo, walipiga shagwe za kutosha
kwa Wemahuku wakidai ndiye mke halali wa Diamond hivyo kumshangilia kila
alipokuwa akiinuka kufanya tukio.Kwenye ukumbi huo, kila kitu kilikuwa
kimeshalipiwa hivyo waalikwa wote walikunywa, kula na kucheza kwa
gharama za Diamond.
Diamond
Platnumz na Wema Sepetu wakiwa wamepozi. Pia kulikuwa na bendi
mbalimbali zilizotumbuiza hasa Ya Moto Band na wasanii mmojammoja au
kundi huku kukiwa na mastaa wengi wa filamu na muziki Bongo ambao
walibaki midomo wazi kutokana na namna shuguli hiyo ilivyokuwa kubwa.
Mapaparazi wetu; Shani Ramadhani, Denis Mtima, Mayasa Mariwata na
Mpiga Picha Mkuu, Richard Bukos walikuwepo ukumbini hapo kuhakikisha
wananasa kila tukio lililotokea na hivi ndivyo mambo yalivyokuwa;
Wema Sepetu akimuweka sawa mpenzi wake. Saa 3:30 USIKU BUKOS AZINGUA
Risasi Jumamosi: Bukos naamini utakuwa umeshafika ukumbini, nini kinaendelea hapo?
Bukos: Kiongozi wangu nipe dakika 20 nitakuwa nimeshafika hapo.
Risasi Jumamosi: Bukos unazingua, ngoja nimcheki Shani ameniambia
ameshafika. Shani kama unanisikia, nini kinaendelea ukumbini hapo?
Baadhi warembo waliohudhuria sherehe hiyo ya Bethidei. SAA 4:00 USIKU BIA ZAMWAGWA
Shani: Kiongozi hapa naona wageni waalikwa tayari wameanza kutembezewa bia za kumwaga, bia zinamwagika kama vile bomba la mvua.
Risasi Jumamosi: Mh! Mapema yote hiyo, si watazima hao? Enhe, nini kinaendelea?
Shani: Kiongozi namuona Vanessa Mdee ‘V-Money’ kaingia hapa, amevaa
kivazi cha ajabu kweli. Cheni ya kiunoni njenje.Risasi Jumamosi: Mh!
Mtoto ana balaa huyo, poa piga kazi Shani, ngoja nimcheki Denis.
Mc wa shughuli hiyo, Sauda Mwilima na 'Chid Benz' wakiwa jukwaani. SAA 5:00 USIKU SHILOLE, NUH FULL MAHABA
Denis: Kiongozi nawaona Shilole na Nuh Mziwanda wameongazana
wanakwenda kuketi lakini hapa full mahaba au mahaba nikongorowe, kila
mmoja anamdekeza mwenzake.Risasi Jumamosi: Safi, hayo ndiyo mahabati,
hebu ngoja nimpe nafasi Mayasa naona anasumbua kweli. SAA 5:45 USIKU
DIAMOND, WEMA WATINGA
Mayasa: Mkuu Diamond na ubavu wake, Wema au Madam ndiyo wanaingia kwa
staili ya kumbikumbi. Pembeni yao namuona mama Diamond naye anawapa
kampani. Duh! Tayari Diamond amefikia kufungua shampeni, waalikwa full
kelele.
Nuh
Mziwanda na mpenzi wake Shilole wamehudhuria sherehe hiyo. Risasi
Jumamosi: Mayasa acha mbwembwe, kwanza niambie keki zipo ngapi na
shampeni?
Mayasa: Keki kubwa zipo tatu, shampeni zipo zaidi ya kumi. Keki ndogo ndiyo zipo za kumwaga, hazina idadi.
SAA 6:20 USIKU NGOMA ZA ASILI
Denis: Sasa ni zamu ya ngoma za asili zinapigwa…Duh! Mzuka umempanda
Diamond ameinuka ameanza kucheza na Wema. Waalikwa full kushangilia,
wanaonesha kuzirudi ngoma za asili hatari.
Wageni
waalikwa wakizidi kuingia ukumbini. Hapa wasanii kibao wameanza kutoa
shangwe, namuona Vincent Kigosi ‘Ray’, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Queen
Darlin, Petit Man, Chegge, Temba, Yamoto Band, Jacob Steven ‘JB’ na Aunt
Ezekiel wanakula bata.
Risasi Jumamosi: Enhee…Denis: Mama Diamond naye kaingia kucheza…
SAA 7:00 USIKU KEKI YAKATWA
Bukos: Keki ndiyo inakatwa, Diamond amekata, anaanza kuwalisha wageni mbalimbali. Ameanza mama Diamond, amefuata Wema sasa.
Keki
ya Bethidei ya Diamond. Analishwa kwa staili ya njiwa. Anamalizia na
wageni mbalimbali wakiwemo waliozaliwa siku moja nay eye ambao siyo
mastaa.Risasi Jumamosi: Bukos muda umekwenda, yaweke matukio yote kwa
pamoja utupe uhondo mzima.
Baada ya nusu saa…
Bukos: Kimsingi rekodi imeandikwa. Bethidei hii watu wamekunywa,
wamekula, bendi mbalimbali zimetumbuiza. Kubwa zaidi, Diamond amepewa
gari aina yaBMW kama lile la Wema na menegimenti yake ya Wasafi.
No comments:
Post a Comment