Diwani wa Kata ya Sokon II wilaya ya Arumeru,Kendo Laizer akizungumza kwenye mkutano huo na kuwataka wananchi kuunga mkono jitihada wa wadau wengine kwa kuchangia ukarabati wa Shule hiyo. |
Meneja Uendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii(NSSF)Jackton Ochieng akizungumza katika hafla .
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Sekei wakishangilia baada ya kukabidhiwa hundi hiyo na vifaa mbalimbali kwaajili ya maendeleo ya Shule hiyo. |
Mbunge wa Arumeru Magharibi mkoani Arusha,Godluck Ole
Medeye akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa NSSF ,viongozi mbalimbali na
walimu wa Shule za Sekei na Naurei. |
Na Mwandishi Wetu,Arumeru
Mfuko
wa hifadhi ya Jamii wa NSSF umetoa msaada wa Sh.10 milioni kwaajili ya
kukarabati Shule ya Msingi kongwe ya Sekei inayotimiza miaka 70 tangu
kuanzishwa kwake.
Akikabidhi
mfano wa hundi hiyo leo,Meneja Uendeshaji wa NSSF mkoa wa
Arusha,Jackton Ochieng amesema wametoa mchango huo kutokana na kutambua
umuhimu wa elimu katika jamii.
Pia
amewataka wananchi kujifunza namna mifiko ya hifadhi ya jamii
inavyofanya kazi zake ili waweze kunufaika na mafao mbalimbali yakiwemo
ya Elimu,Uzazi,Mazishi,Kuumia kazini na mengine.
Kwa
upande wake Mbunge wa Arumeru Magharibi,Godluck Ole Medeye alimshukuru
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,Dk Ramadhan Dau kwa kukubali kuchangia ukarabati
wa Shule hiyo ambayo ni ukombozi kwa jamii ya eneo hilo.
"Ili
tuwe na taifa endelevu hatuna budi kuwajengea wanafunzi mazingira
mazuri ya kujifunzia ili tujihakikishie kuwa na wataalamu katika fani
mbalimbali ambazo ni msingi wa maendeleo."amesema Ole Medeye
Katika
hatua nyingine mbunge huyo amewahimiza wananchi kujiandikisha kwenye
daftari la makzi ili kupata haki ya kupiga kura katika uchaguzi wa
serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment