Uvumilivu
wa kusubiri mwanaume wa kuja kumpigia goti na kumuuliza ‘will you marry
me?’, umemshinda mwanamke mmoja wa Uingereza, aliyeamua kuchukua uamuzi
wa kujichumbia na kujioa mwenyewe!
Grace
Gelder ambaye ni ‘mme na mke’ alijichumbia November, 2013 na baadae
kujioa March, 2014 na kuamua kufanya sherehe ya harusi yake
iliyohudhuriwa na wageni 50.
Na ule wakati wa ile hatua ya ‘you may now kiss the bride’ ulipowadia, Grace alijibusu kwenye kioo.
Mwanamke huyo alisema baada ya kuwa single kwa miaka 6 aliamua
ku-fall in love na ‘yeye mwenyewe’ baada ya kuona hapati mtu wa
kumpenda.
Mwanamke huyo alisema kuwa pia wimbo wa Björk song Isobel ambao una
mstari unaosema ‘My name’s Isobel, married to myself’, nao
ulimuhamasisha kutimiza azimio lake.
Source: Mirror
No comments:
Post a Comment