Kundi la
wanamgambo wa kiislamu la Islamic state limetoa mkanda wa video
unaoonyesha mateka Alan Henning raia wa Uingereza akikatwa kichwa.
Henning mwenye umri wa miaka 47 ambaye ni dereva wa texi kutoka
kaskazini mwa Uingereza alitekwa nyara mwezi Disemba mwaka uliopita
alipokuwa akilifanyia kazi shirika moja la kutoa huduma za misaada kwa
wakimbizi nchini Syria.
Kundi la Islamic State ambalo limechukua udhibiti kwenye maeneo ya
mpaka kati ya Syria na Iraq tayari lishawaua waandishi wa habari raia wa
Marekani James Foley na Steven Sotlof pamoja na mfanyikazi wa kutoa
huduma za misaada kutoka Scotland David Haines.
Mapema babake John Cantlie raia wa Uingereza ambaye anashikiliwa
mateka na wanamgambo wa Islamic State aliomba kuachiliwa kwa mwanawe.
No comments:
Post a Comment