Viongozi
wa Afrika wanaokutana mjini Paris Ufaransa wamekubaliana kutangaza vita
dhidi ya kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram.
Rais
wa Ufaransa, Francois Hollande ambaye ni mwenyeji wa mkutano huo,
amesema kuwa mataifa ya kikanda yameahidi kushirikiana na kuarifiana
taarifa za kijasusi kuhusu kundi hilo ili kupambana nalo.
Mwezi
jana kundi hilo liliwateka nyara zaidi ya wasichana miambili Kaskazini
Mashariki mwa Nigeria ambako kundi hilo linaendeshea harakati zake.
Inaarifiwa kuwa kundi hilo lilifanya mashambulizi mapya usiku kucha nchini Nigeria na Cameroon.
Maelfu
ya watu wameuawa na wengine kuachwa bila makao kutokana na vita ambavyo
vimekuwa vikiendeshwa na Boko Haram katika miaka ya hivi karibuni.
Mkutano
uliofanyika mjini Paris, ulihudhuriwa na mwenyeji Rais Francois
Hollande, Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan, na marais wenzao kutoka
Benin, Cameroon, Niger na Chad.
Baada
ya mkutano huo bwana Hollande alisema washiriki wa mkutano huo,
wamefikia mwafaka wa kimataifa na mkakati wa kikanda kupambana na kundi
hilo.
Alisema
kuwa mkakati huo utahusisha kushirikiana kijasusi , uchunguzi wa
mipakani na kuwepo kwa vikosi vya nchi hizo katika maeneo ya mipakani na
katika eneo linalozingira ziwa Chad pamoja na kutafuta uwezo wa
kukabiliana na mashambulizi yanayofanywa na wapiganaji hao.Chanzo BBC
Swahili
No comments:
Post a Comment